Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- WAKAZI MTAA WA KATI SOWETO MBEYA WAINGIA MTAANI WAJITENGENEZEA BARABARA ILIYOHARIBIWA NA MVUA
- WATENDAJI WA UBORESHAJI WA DAFTARI LINDI, MTWARA, RUVUMA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI
- MAFUNZO UBORESHAJI WA DAFTARI MIKOA YA MTWARA, LINDI NA RUVUMA YAFUNGULIWA LEO
- DROO YA MASTA BATA YA BENKI YA NMB KUWAPELEKA WATEJA WAKE KULA BATA DUBAI
- Jinsi nilivyoweza kupata mchumba toka nchini Marekani
- MATAPELI CCM WABAINIKA,NI WALE WANAOPITA KUOMBA FEDHA BILA RIDHAA YA CHAMA,WATANGAZIWA KIAMA CHAO
- MH. MAHUNDI VIJANA TUACHE KUTUMIA MITANDAO VIBAYA
- Bosi wangu anang’ang’ania kuzaa mtoto na mke wangu!
Author: Mbeya Yetu
Madiwani wa Viti Maalum Jiji la Mbeya na Mbeya Vijini wametembelea miradi miwili ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya.Akitoa taarifa mbele ya Madiwani hao Afisa Uhusiano Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya Neema Stanton amesema lengo la ziara hiyo ni kuielezea miradi mbalimbali inayotekelezwa ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyoanza machi 16,2024 na kilele chake ni machi 22,2024.Aidha Afisa Uhusiano wa Mamlaka ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji ukiwemo mradi mkubwa wa Kiwira utakaogharimu…
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wafanyabiashara kumi kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu. Akitoa taarifa Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watu kumi wanahusishwa na tukio hilo Ilomba Jijini Mbeya. KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHAB Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wafanyabiashara kumi kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu. Akitoa taarifa Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watu kumi wanahusishwa na tukio hilo Ilomba Jijini…
Taasisi ya Tulia Trust imetoa Msaada wa Viti Mwendo Vinne (4) kwa Watu Wenye Uhitaji Maalumu (Watu wenye Ulemavu) kata ya Itezi Jijini Mbeya. Zoezi hilo la kukabidhi viti mwendo limefanyika katika Uwanja wa Gombe likiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji Mhe.Mubarak Alhaji Batenga akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Mhe. Beno Malisa. TULIA TRUST YAWAPA TABASAMU WANA-ITEZI Taasisi ya Tulia Trust imetoa Msaada wa Viti Mwendo Vinne (4) kwa Watu Wenye Uhitaji Maalumu (Watu wenye Ulemavu) kata ya Itezi Jijini Mbeya. Zoezi hilo la kukabidhi viti mwendo limefanyika katika Uwanja wa Gombe likiongozwa…
Kaimu Mtendaji Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya Mhandisi Barnabas Konga katika maadhimisho ya wiki ya maji iliyoanza machi 16,2024 ameendelea kutolea taarifa miradi mbalimbali inayotekelezwa na Mamlaka taarifa iliyoambatana na ziara ya kuitembelea miradi hiyo ukiwemo mradi mkubwa wa Kiwira utakaogharimu shilingi bilioni 250 unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maji ambapo Kampuni ya China Railway Connstuction ndiyo imepewa kandarasi chini ya Mhandisi Mshauri Kampuni ya GKW Consultant awamu ya kwanza zitatumika shilingi bilioni 119. Konga amesema Jiji la Mbeya na Mbalizi lina vyanzo ishirini ambavyo vinazalisha lita milioni 66.5 kwa siku wakati uhitaji…
Shirika la kimataifa la HJMRI limesema linatarajia kutoa Sh 500 milioni kuwezesha mabinti balehe na wasichana vijana kupitia mradi wa dreams kwa ufadhiri wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na Ukimwi (PEPFAR) Mkurugenzi Mkuu wa HJFMRI Tanzania , Sally Chalamila amesema Machi 16 mwaka huu wilayani Kyela wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa mbalimbali na mashine za kisasa vyenye thamani ya Sh 178 milioni .Mashine na vifaa hivyo vimetolewa na Shirika la HJFMRI kupitia WRAIR -DOD kwa ufadhiri wa Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani (PEPFAR) kwa kushirikiana na Asasi ya Tumaini.Akizungumza kwa niaba…
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh: Kasim Majaliwa Majaliwa tayari amewasili katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe ulioko Mkoani Mbeya na Kupokelewa na Mwenyeji wake Cde: Juma Z. Homera Mkuu wa Mkoa wa Mbeya kwaajiri ya kushiriki Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani Leo Tarhe18 March 2024 ambalo Kitaifa linafanyika Jijini Mbeya katika Ukumbi wa Eden Highlands Hotel.
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amemuagiza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Rebman Ganshonga, kuhakikisha anapeleka huduma ya maji kwenye vitongoji ambavyo bado havina huduma ya maji. Mhandisi Mahundi ametoa maagizo hayo leo Machi 17, 2024 akiwa katika muendelezo wa ziara ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya kukagua utekelezaji wa miradi ya Maji Mkoani Ruvuma Akiwa ziarani pia Mhandisi Mahundi ametoa rai kwa wananchi kuendelea kutunza vyanzo vya maji ili miradi ya maji iwe endelevu. *WANANCHI ELFU 9,659 KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MALUNGU NYASA* NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi…
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujidhatiti katika utangazaji utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Utalii nchini. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameyasema hayo leo Machi 17,2024 wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya TTB jijini Dar es Salaam . TTB YATAKIWA KUJIDHATITI UTANGAZAJI UTALII NCHINI Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujidhatiti katika utangazaji utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Utalii nchini. Mwenyekiti…
WANANCHI MBEYA WALIA KUVAMIWA NA TAZARA
Wakazi wa Iyunga,Ivumwe,ltuha,ltezi na Nsalaga Jijini Mbeya wameiomba Serikali kutolea ufafanuzi mgogoro wa ardhi baina yao na Shirika la Reli Tanzania na Zambia(TAZARA)baada ya Shirika hilo kuweka mawe(Bicons)katika maeneo yao sanjari na kuwataka wabomoe nyumba zao zinazodaiwa kuwepo mita hamsini ndani ya hifadhi ya reli kinyume na makubaliano.
Wananchi hao kwa nyakati tofauti wakiwa na nyaraka mbalimbali kuhusiana na mgogoro huo wamepaza sauti zao baada ya kugonga ukuta ofisi zote ikiwemo TAZARA na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya.
Maadhimisho ya wiki ya maji yameanza machi 16,2024 ambayo yatahitimishwa machi 22,2024 kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya kufanya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa Jijini Mbeya na Mbeya Vijijini. Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo kwa Waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ambaye pia ni Mkurugenzi wa uzalishaji maji na usambazaji maji safi na usafi wa Mazingira Mhandisi Barnabas Konga amesema Wizara ya Maji imekuwa ikiratibu maadhikisho hayo kila mwaka kutekeleza azimio la Umoja wa Mataifa namba 47. Konga ameitaja baadhi ya miradi inayotekelezwa ambapo katika kipindi cha miaka mitatu upatikanaji wa…