Author: Mbeya Yetu

#mbeyayetutv
Wakili Msomi na Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kapteni Sambwee Shitambala Mwalyego amejitokeza kuchukua fomu kuwania Ubunge Jimbo la Mbeya mjini.

Shitambala amesema ameguswa kuwania nafasi hiyo akitumia haki yake ya msingi, akidhamiria kuendeleza pale alipoishia Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson ambaye amehamia kuwania katika jimbo jipya la Uyole.

Read More

Kada wa Chama cha Mapinduzi, CPA (T) Ruth Hassani akisaini kitabu. Kada wa Chama cha Mapinduzi, CPA (T) Ruth Hassani  ametia nia ya kuwania kuteuliwa na Chama chake kuwania Ubunge katika Jimbo la Same Mashariki, Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro. Akiwa ameambatana na Mumewe Bw. Banyinga Majeshi, CPA Ruth ambaye ni Mhasibu wa Chuo Kikuu cha Sokoine (SUA) mkoani Moprogoro alichukua fomu hiyo katika Ofisi za CCM Wilaya ya Same  na kukabidhiwa na Katibu wa CCM Wilaya, Ndg.Amos Kusakula leo Juni 29,2025. Ruth amesema nia yake si kutafuta nafasi ya uongozi katika jimbo la Same Mashariki bali kuwasemea Wanasame Mashariki…

Read More

Wananchi wa Jimbo la Uyole, Mkoani Mbeya, kwa moyo wa upendo na imani kubwa, wamemchukulia fomu ya kuwania tena Ubunge Dkt. Tulia Ackson @tulia.ackson kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba 2025. Hatua hiyo inaonesha wazi dhamira ya wananchi kuendelea kumuunga mkono kiongozi huyu mahiri ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa jimboni humo.

Wakizungumza baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, baadhi ya wakazi wa Uyole wamesisitiza kuwa Dkt. Tulia ni chaguo sahihi kutokana na utendaji wake uliotukuka, uwezo mkubwa wa kiuongozi na ushirikiano wake wa karibu na wananchi katika kutatua changamoto mbalimbali.

Kwa kauli moja, wananchi hao wameahidi kuendelea kumpigania hadi ushindi, wakiamini kuwa uongozi wake utaendeleza kasi ya maendeleo na kuimarisha ustawi wa wananchi wa Uyole.

Read More