Author: Mbeya Yetu

#Aipongeza kwa kuwafungulia barabara wakulima Dodoma Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Bi. Asia Messos ameipongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa ujenzi wa miundombinu ambayo imeweza kuwasaidia wakulima kusafirisha mazao yao kwa wakati. Ameyasema hayo mara baada ya kutembelea banda la TARURA kwenye Maonesho ya NaneNane Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma. Amesema kwamba kazi kubwa imefanyika katika maeneo mengi na hivyo wameweza kuwarahisishia wakulima kusafirisha mazao yao kwa wakati na kufikisha kwenye masoko. “Niwapongeze sana TARURA kwa kazi kubwa mnayoifanya vijijini,sisi ni mashahidi katika maeneo yetu,wakulima wanaweza kusafirisha mazao na bidhaa zao…

Read More

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa zaidi ya wakulima 18,000 wanatarajiwa kunufaika moja kwa moja na Mpango wa Taifa wa Kilimomisitu ifikapo mwaka 2031, ambao unalenga kuhakikisha wakulima milioni 15 wanatumia teknolojia na mbinu bora za kilimomisitu nchini. Mkakati huo uliozinduliwa mwaka 2024 na Mhe Dkt. Philipo Isdori Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umejikita katika kuendeleza kilimomisitu nchini, ikiwa na dhima ya kukuza ufanisi wa mbinu za kilimomisitu na teknolojia zake ili ziweze kutumika na jamii ya wakulima kwa ajili ya kudumisha ustawi wa jamii, uchumi na mazingira. Akizungumza…

Read More

Ujumbe wa Bodi ya Shirika la Kimataifa la Helen Keller tarehe 5 Agosti, 2025 pamoja na masuala mengine ulifika Isman Wilaya ya Iringa kujionea kwa vitendo zoezi linaoendelea la kambi ya upasuaji wa ugonjwa wa macho ujulikanao kama mtoto wa jicho kambi itakayo toa huduma hiyo kwa siku saba. Akiongea wakati wa kikao kifupi ofisi ya mkuu wa mkoa mkoani Iringa kabla ya kutembelea kituo hicho, Rais wa shirika hilo Sarah Bochie amesema shirika hilo limeamua kutembelea mkoani Iringa ili kujionea na kujiridhisha huduma zinazotolewa kwa vitendo kwani shirika lake linafanya kazi kwa kanzi data na takwimu ili kutoa tathimini…

Read More

Rais wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa kitabu Ndoto ya Yatima kilichoandikwa na Shukurani Gideon Mwasanjobe, Mkurugenzi wa Tehla Foundation (TEFO) na mmiliki wa Shule ya Sekondari Vanessa. Uzinduzi huo utafanyika Septemba 13, 2025 jijini Mbeya.

Kwa kaulimbiu “Tambua Thamani ya Ndoto Iliyojificha Ndani ya Yatima”, kitabu hiki kinalenga kuibua ari na matumaini kwa watoto yatima. Mratibu wa tukio, George Mwaitenda, amesema uzinduzi huo utahusisha ushuhuda kutoka kwa watoto waliowahi kunufaika na malezi ya taasisi za TEFO na Shury Agri Farm Ltd.

Zephania Gideon Kang’anga, Mkurugenzi wa Shury Agri Farm Ltd, amesema taasisi yao kwa kushirikiana na TEFO inalenga kusaidia watoto yatima kutambua na kutimiza ndoto zao kupitia elimu na ujasiriamali.

Kwa upande wake, Katibu wa Asasi za Kiraia Jiji la Mbeya, Mustafa Namnenje, amepongeza juhudi za Mwasanjobe kuwekeza katika maisha ya watoto yatima, huku akiitaka jamii kuunga mkono jitihada hizo.

Mwalimu Andrew Ezekiel Wihala, mlezi wa watoto yatima, amesisitiza kuwa tukio hilo lina umuhimu wa kijamii kwani linawakumbusha Watanzania wajibu wa kuwatunza na kuwawezesha watoto waliopoteza walezi wao.

Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi, Emmanuel Mwambelo, pamoja na Benson Thom na Deborah Emmanuel, wamezitaka taasisi na wadau kuunga mkono na kudhamini tukio hilo la kihistoria litakalogusa maisha ya we

Read More

Na Mwandishi Wetu  Agosti 3, 2025 — Wazalishaji wa maudhui mtandaoni wametakiwa kuepuka kuchapisha taarifa zinazoweza kusababisha taharuki au kuchochea machafuko, hususan katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu. Wito huo umetolewa na Meneja wa Kitengo cha Huduma za Utangazaji kutoka TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka, alipokuwa akiwasilisha mada katika mkutano wa watoa maudhui mtandaoni ulioandaliwa na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC). Mhandisi Kisaka amesema kuwa kipindi cha uchaguzi huwa na hali ya migawanyiko, mivutano na upotoshaji mkubwa, hivyo ni muhimu mabloga na watoa maudhui wengine kujiepusha kusambaza uvumi, kutangaza kwa umakini,…

Read More

Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Kata jijini Mbeya wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi ili kuepusha vurugu wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu.

Tahadhari hiyo imetolewa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Anamary Joseph, anayesimamia majimbo ya Mbeya Mjini na Uyole, wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi wa kata hizo.

Afisa Uchaguzi wa Jiji la Mbeya, Gregory Emmanuel, amesisitiza umuhimu wa wasimamizi hao kuwa na nyaraka muhimu kama Katiba na kanuni za uchaguzi ili kusimamia kikamilifu utoaji na urejeshaji wa fomu za wagombea pamoja na ratiba ya kampeni.

Washiriki wa mafunzo hayo wameonesha utayari wao kutekeleza majukumu kwa weledi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu

Read More