Author: Mbeya Yetu

Diwani wa Kata ya Ilomba, Ndg. Noah Edson Mwakisu, leo amerejesha fomu za kuwania Umeya wa Jiji la Mbeya kupitia CCM. Akizungumza katika Ofisi za CCM Mbeya Mjini, Mwakisu alisema anagombea nafasi hiyo ili kulipa jiji mwelekeo mpya wa maendeleo, akisisitiza umuhimu wa uongozi wenye maono, ushirikiano na uwajibikaji.
Mwakisu alisema Mbeya ina fursa kubwa za kimaendeleo kutokana na mazingira na jiografia yake, hivyo inahitaji kiongozi anayeendana na mahitaji ya kizazi cha sasa, hususan vijana ambao ndio nguvu ya uchumi wa jiji. Aliomba sapoti na baraka za wananchi, akiahidi kulifanya jiji hilo mfano wa kuigwa endapo atapewa dhamana.
Kurejesha fomu hizo kunamweka rasmi katika kinyang’anyiro cha ndani ya CCM cha kuwania Umeya wa Jiji la Mbeya mwaka huu.

Read More

Kijana Golden Kidumba, maarufu kama DON. G, amewagusa watoto wa mitaani kwa kuwapatia chakula, kuwanunulia nguo na kutumia muda wa siku nzima akiwa nao, ikiwa ni sehemu ya jitihada zake za kuikumbuka jamii aliyotokea.

Golden, mzaliwa na mkazi wa zamani wa Njombe, anasema maisha magumu aliyoyapitia utotoni ndiyo yamemfanya kuwa na moyo wa huruma na kujitoa kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.

“Nimekulia kwenye maisha magumu sana. Lakini namshukuru Mungu kwa kunibariki na kunifanya niweze kuwakumbuka hawa wadogo zangu wa mitaani. Nimekula nao, nimesherehekea nao na pia nimewanunulia nguo ili wajisikie wanathaminiwa kama watoto wengine,” amesema DON. G.

Amesema kusaidia watoto wa mitaani si tukio la leo pekee, bali ni jambo alilolianza miaka kadhaa iliyopita, ikiwemo kutembelea hospitali na kuwasaidia watu wenye uhitaji.

Golden ameweka wazi kuwa ndoto yake ya baadaye ni kuanzisha taasisi ya msaada na hata kujenga shule maalum kwa ajili ya watoto hao, ili kuwapa elimu, malezi na fursa za kuanza maisha mapya.

Baadhi ya watoto wa mitaani waliopokea msaada huo wameeleza machungu ya maisha yao, ikiwemo vipigo, njaa, manyanyaso na mara nyingi kudharauliwa kama wahalifu bila kujua historia zao.

Kijana Brian Edwin, anayelelewa katika kituo cha Mtama, amesema:
“Maisha ya mitaani ni magumu. Tunapigwa, tunanyanyaswa na tunaishi bila uhakika. Lakini leo tumepata faraja kubwa kutoka kwa DON. G. Mungu ambariki.”

Wengine kama Anody Nyondo na Gifty wameeleza jinsi walivyokimbia nyumbani kutokana na migogoro ya kifamilia na manyanyaso, hali iliyowalazimu kuingia mitaani.

Watoto hao wameiomba jamii na serikali kutowatenga, bali kuwaona kama watoto wanaohitaji msaada na si wahalifu.

Golden ameendelea kutoa wito huo huo:
“Tusishikilie mali bila sababu. Tukiondoka duniani, hatuchukui chochote. Tuwakumbuke watoto wa mitaani; wanahitaji upendo na msaada wetu.”

Read More

Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba leo Novemba 17, 2025 amekabidhiwa Ofisi na Waziri Mkuu Mstaafu Kassim Majaliwa, Mlimwa Jijini Dodoma Novemba 17, 2025.

Viongozi waliohudhuria hafla ni pamoja na Naibu Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. Doto Biteko, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi, Wakuu wa Idara na watumishi wengine wa Ofisi ya Waziri Mkuu.

Read More

Taasisi ya Tulia Trust iliyo chini ya Mbunge wa jimbo la Uyole jijini Mbeya Dkt Tulia Ackson, wameanza ujenzi wa nyumba ya famikia ya mzee Anyomwisye Mwalyaje mkazi wa mtaa wa Mwafute kata ya Ilemi iliyoteketea kwa moto usiku wa September 5 kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa Umeme.

Ujenzi huo umeanza baada ya Mbunge wa jimbo la Uyole kutoa ahadi ya kumjengea nyumba mzee Anyomwisye Mwalyaje alipomtembelea kutokana na kadhia ya nyumba yake kuteketea kwa moto pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani.

Afisa kutoka taasisi ya Tulia Trust kitendo cha habari Addi Kalinjila amesema ujenzi wa nyumba hiyo unaanza maramoja baada ya vifaa kufika eneo la ujenzi ili kurejesha maisha ya familia hiyo kama yalivyokua hapo awali.

Read More