Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Dkt. Tulia Aongoza kwa Vitendo, Apiga Kura na Kuhamasisha Ushindi wa CCM Uyole
- DKT MARY MWANJELWA AUNGANA NA WANANCHI KUPIGA KURA AHAMASISHA KUJITOKEZA KWA WINGI AMANI IMETAWALA
- Nilivyookoa Ndoa Yangu Baada ya Migogoro Kila Usiku Kuhusu Pesa na Wivu
- MWAKIPESILE: ”TUKAANDAMANE OKTOBA 29 KWA AJILI KUWAPIGIA KURA VIONGOZI KWA AMANI”
- “Tunatiki CCM, Tunatunza Amani” — Kauli ya Bodaboda Kiwira Yakonga Moyo wa Suma Fyandomo
- Nilivyomfanya Mtu Aliyenidharau Kuniheshimu na Kunitegemea Kwa Mambo Mengi
- NABII MPANJI AUTANGAZIA UMMA, WAKRISTO WASISHIRIKI MAANDAMANO WAJITOKEZE KWA WINGI KUPIGA KURA
- Nilivyookoa Biashara Yangu Baada ya Wateja Wote Kupotea Ghafla
Author: Mbeya Yetu
Jumla ya Wilaya 139 Nchini zita fikiwa na huduma ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na mpaka sasa Wilaya 108 tayari zimefikiwa huku Wilaya 31 zilizosalia nazo zikitarajiwa kupata huduma ya mkongo wa Taifa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Pwani alipo tembelea na kukagua Vituo Vya Mkongo vilivyopo Chalinze, pamoja na kituo kipya Cha Mkongo wa Taifa kilicho jengwa Kibaha .
Aidha, Mhe. Mahundi amempongeza na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa namna anavvyo endelea kuiwezesha Sekta hii ya Mawasiliano apa Nchini Kwa kuendelea kuwekeza fedha nyingi katika Shirika la mawasiliano apa Nchini ( TTCL) na kuahakikisha Shirika linakuwa kibiashara pamoja na kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali isibaki kama Kisiwa.
Vilevile, Mhe Mahundi ameeleza kuwa Serikali tayali imetenga fedha Kwa ajili ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuelekea Nchi jiran ya Congo (DRC) kupitia Ziwa Tanganyinga hadi Kalemei na tayali Utekelezaji wake umeshaanza na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka mradi huu utakuwa umekamilika.
Sambamba na hayo, Mhe.Mauhidi amaeleza kuwa kazi kubwa inaendelea kufanyika katika uwekezaji wa Mkongo wa Taifa ikiwa ni pamoja na Kuunganisha Mkongo wa Taifa na Mikongo ya Baharini, kupitia SEACOM, EASSY na 2AFRICA, na kwakuzingatia tunajenga Tanzania ya dijitali tunaunganisha Mkongo wa Taifa na Mikongo ya Baharini iliyopo Mombasa Kenya kupitia HorohoroTanga. Na hii itasaidia kuongeza uhakika wa huduma ya Mawasiliano Nchini.
Endapo mkongo wa Taifa wa Mawasiliano utakamilika utapanua wigo kibiahara ndani na nje ya nchi na kuongeza uchumi wa kidijitali.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambae ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge Jimbo la Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson ametoa Msaada wa Kumsomesha Yohana Japhet anayeishi Kwenye Mazingira Magumu.
Yohana anayeishi na Bibi yake Mlezi Katika Kata ya Ilomba Mtaa wa Ituha Mbeya Mjini anasoma Darasa la Saba hapo awali alikuwa akifanya Kazi ya Kuponda Kokoto Ili apate Fedha Kwaajili ya kununua Mahitaji Mbalimbali ya Shule na Chakula.
Mhe. Dkt. Tulia Ackson amemtembelea Kijana huyo na Kuahidi Kumsomesha hadi atakapofikia ukomo wa Masomo yake pia amemsaidia Bibi yake Chakula (Mchele Kilo 40) na Mavazi (Nguo na Blanket).
Jina langu ni Halima, nimekuwa kwenye ndoa kwa miaka mitano sasa, hakika naweza kusema mimi ni miongoni mwa wanawake ambao wamefaidi matunda ya ndoa vilivyo, sijawahi kukumbana na kadhia yoyote ile. Watu wengi husema kuwa ndoa ni ngumu na hii ni kutokana na wanaume wengi kutokuwa waaminifu katika ndoa zao kwani baada ya kipindi fulani huanza kutafuta wanawake wengine wa nje kwa madai ya kubadilisha ladha. Lakini pia hata baadhi ya wanawake nao wamekuwa na tabia hiyo tena kwa sana ila wamekuwa wakifanya kwa siri kubwa kiasi ni vigumu kwa waume zao kuwabaini kwa wepesi. Wakati naolewa na mume wangu…
Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao”.
Jina langu ni Fatma mkazi wa Pwani, Kenya, baada ya mimi kuzaliwa, baba na mama yangu walitengana na baba yangu alioa mke mwingine, wakati huo mimi nilikuwa nalelewa na mama yangu hadi pale nilipotimiza miaka saba ndio nikaenda kwa baba yangu mzazi. Basi niliishi na baba na mama yangu wa kambo kwa shida sana kwani hakuwahi kunipenda hata siku moja, lakini namshukuru ingawaje niliishi kwa changamoto lakini sikuwahi kukata tamaa ya kuishi hapa duniani. Kiukweli nilipitia kila aina ya manyanyaso na masimango, hakuna neno baya ambalo sijawahi ambiwa, kuhusu manyanyaso hakuna rangi sijawahi kuyaona ila sikukata tamaa. Dunia ilizidi kuwa…
Mkuu wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera ametembelea Gereza la Ruanda lililoko Jijini Mbeya na Kuzungumza na wafungwa ikiwa ni Pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili.
RC Homera amewaasa wafungwa hao kuhakikisha wanajifunza ujuzi mbalimbali wawapo hapo ili watakapopata ridhaa ya kurudi uraiani wautumie kuendesha maisha yao na kuwa walimu wa wengine.
Awali Wakieleza Maombi yao kwa RC Homera wamemuomba awahimize Viongozi wa Serikali kufika gerezani hapo kuwatembelea kwakuwa kufika Kwao wao hupata faraja kuu na kuamini kuwa serikali iko pamoja nao.
“Tunakushukuru sana kwa kuja Mkuu wa Mkoa Mimi nimefika hapa 2015 sijawahi kuona Kiongozi Mkubwa anakuja kututembelea, ujio wako tuna imani kuwa liko tumaini kubwa mbele yetu” amesema mmoja wa Wafungwa.
Mbali na hayo wafungwa pia wamemuomba RC Homera kuwasaidia kumleta Dkt: Tulia Ackson spika wa bunge la Tanzania na mbunge wa Mbeya Mjini kadharika Mganga Mkuu wa Mkoa.
“Mh: tusaidie kumuomba Rais wa mabunge Duniani na Spika Dkt: Tulia Ackson aje atutembelee maana yule ndio Mbunge wetu hata kama hatutokei hapa lakini tayari tuko kwenye Ardhi yake aje atuone”
“Pia Mganga mkuu wa mkoa tunamuomba aje atuone maana tunayo mengi ya kuzungumza naye hasa kuhusu magonjwa mbalimbali yanayotusibu”
Baada ya kusikiliza changamoto hizo Mkuu wa Mkoa ameahidi kuyatendea kazi kwa haraka hasa kuwaleta Viongozi wote sawasawa na maombi yao.
Lakini pia ametoa Kiasi Cha Shilingi Milioni Moja kwaajiri ya Kununua Chakula (nyama) Msaada ambao umeambatana na magodoro yaliyotolewa naM/kit UVCCM Mkoa wa Mbeya Yasin Ngonyani kwa Kushirikiana na mfanyabiashara Achimwene.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu) Dkt. Rose Likangaga akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mjumbe wa Tume, Dkt. Zakia Mohamed Abubakar. Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari na Elimu ya Mpiga Kura (Elimu) Dkt. Rose Likangaga akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mjumbe wa Tume, Dkt. Zakia Mohamed Abubakar. Mwenyekiti wa Mafunzo, Bw. Khalid Khalif akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo. Na Mwandishi wetu, Songea Watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga kura mkoani Ruvuma wametakiwa kuhamasisha wananchi wenye sifa ili wajitokeze kujiandikisha na kupata haki yao ya kikatiba itakayowawezesha…

 
		