Author: Mbeya Yetu

Taasisi ya Tulia Trust imetoa mifuko mia nne kwa shule tatu za msingi na sekondari Jijini Mbeya kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya madarasa katika shule hizo. Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na Shule ya Msingi Mlimani iliyopo Kata ya Sinde,Sekondari ya wasichana ya Dkt Tulia ilioyopo Kata ya Iyunga na Sekondari ya Itende inayomilikiwa na Jumuia ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)iliyopo Kata ya Itende Jijini Mbeya. Shule ya msingi ya Mlimani iliyopo Kata ya Sinde Jijini Mbeya imepokea msaada wa mifuko mia mbili kutoka Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Dkt Tulia Ackson Rais wa Mabunge Duniani Spika…

Read More

Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimali watu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Miriam Mmbaga amefungua Kikao cha Baraza Dogo la Wafanyakazi Jeshi la Zimamoto na Uokoaji nchini Kikao kilichofanyika Jijini Mbeya akiwataka wafanyakazi kufanya kazi kwa uadilifu na kufika kwa wakati eneo la tukio. Kamishina Utawala na Fedha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mbaraka Semwanza amesema Jeshi la Zimamoto limeendelea kufanya maboresho mbalimbali pamoja na kutoa elimu kwa jamii ambapo serikali imewaongezea vifaa vya kukabiliana na matukio ya ajali kwa kuwapatia magari kumi na mbili ya Zimamoto ambayo yatagawiwa kwenye mikoa mbalimbali. Charo Mangare Kaimu Kamishina wa Opesheni ambaye amesema wamepokea…

Read More

Meneja wa Wakala wa Barabara nchini(TANRODS)Mkoa wa Mbeya Mhandisi Masige Matari amesema miradi mbalimbali ya barabara inayotekelezwa Mkoani Mbeya katika uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imefungua fursa za kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Mbeya na nchi jirani.Masige ameyasema hayo katika mkutano wake na Waandishi wa Habari Mkoani Mbeya huku akiitaja mitandao mbalimbali ya barabara za TANROADS ambazo inatekelezwa ni kuwa jumla ya kilometa 1,403.3 ambapo kati ya hizo kilometa 469.3 ni barabara za lami na kilometa 934 ni za changarawe. Ameitaja baadhi ya miradi ya barabara za lami kuwa ni pamoja mradi wa njia nne kuanzia Nsalaga-lfisi…

Read More

Baadhi ya watendaji ngazi ya Kata na kijiji Tarafa ya Ilongo wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya wamekuwa wakilalamikiwa na wananchi kwa kutokutekeleza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kutokusoma taarifa ya mapato na matumizi ya kila baada ya miezi mitatu.Hayo yamebainishwa na afisa tarafa hiyo Bi Magdalena Sikwese alipokuwa kwenye kikao cha kiutendaji amesema amepokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakilalamikia baadhi ya watendaji hawaweki wazi mapato ya vijiji kwa kuitisha mikutano na kueleza mapato yametumikaje. Watendaji wa vijiji tunalala kwenye Maeneo yetu,tunasahau wajibu wetu wa kusoma Mapato na matumizi mpaka Wananchi wanalalamika sana mnatakiwa msome Mapato na matumizi Yani tekelezeni majukumu…

Read More

Serikali imekamilisha ujenzi wa daraja linalounganisha Kata ya Minyughe na Makilawa, katika wilaya ya Ikungi mkoani Singida, lililokatika miaka mitatu iliyopita, na hivyo kuathiri shughuli za kiuchumi na upatikanaji wa huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu. Kukamilika kwa daraja hilo la chuma (Mibey Bridge) lenye urefu wa mita 30 lililogharimu zaidi ya Sh. Bilioni 1.6/-katika barabara ya Mtamaa-Minyughe hadi Mtavira, Wilayani Ikungi, litaenda kufungua fursa ya kiuchumi kwa wananchi wa kata hızo.Meneja wa Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA), Mkoa wa Singida, Mhandisi Ibrahim Kibasa, alisema kukamilisha uunganishaji wa vyuma kwa ajili ya daraja hilo, kumewezesha mto Minyughe…

Read More

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amefungua rasmi Mkutano Mkuu wa 148 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) uliofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha CICG, Geneva nchini Uswisi leo tarehe 24 Machi, 2024. Mkutano huo unatarajiwa kujadili Dhima Kuu ambayo ni “Matumizi ya Diplomasia ya Kibunge katika kuleta Amani na Maelewano Duniani”. Mkutano huo umehudhuriwa na Maspika wa Mabunge 48 na washiriki zaidi ya 1,500 na unatarajiwa kuhitimishwa tarehe 27 Machi, 2024. Huu unakuwa Mkutano wake wa kwanza kuufungua tangu achaguliwe kuwa Rais…

Read More

#mbeyayetutv
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amevunja ukimya na kuweka mambo hadharani kwa kuelezea hisia zake juu ya kile kinachoelezwa na baadhi ya wanasiasa wilayani’Namtumbo mkoani Ruvuma.
Akiwa katika iftari maalumu iliyoandaliwa na Taasisi ya Site Trust Foudation na Site Fm zinazosimamiwa na wake zake Imani na Jasmin.
‘’Namtumbo ni Nyumbani kwetu Nimezaliwa Namtumbo sijaja kufanya siasa tuwaunge mkono viongozi wetu’’amesema Homera

Read More

Naibu Waziri wa Maji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amezindua mradi wa uchimbaji visima vya maji uzinduzi uliofanyika Kijiji cha Azimio Mapula Kata Kongolo Mswiswi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya ambapo Kata tano zitanufaika na mradi huo Wilaya ya Mbarali. Mahundi amesema visima vingine vitachimbwa katika vijiji vya Mpolo,Iwalanje,lbohola,Limsemi,Nyakazombe na Vikaye. Mahundi amesema Wizara itakamilisha kiasi cha shilingi milioni 96 hivi karibuni kwa lengo la kuukamilisha mradi huo ili mitambo iweze kuhamie Kata zingine nao waonje keki ya Mama Samia Suluhu Hassan. Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mbarali Mhandisi Samwel Heche amesema…

Read More

Madiwani wa Viti Maalum Jiji la Mbeya na Mbeya Vijini wametembelea miradi miwili ya maji inayotekelezwa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya.Akitoa taarifa mbele ya Madiwani hao Afisa Uhusiano Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya Neema Stanton amesema lengo la ziara hiyo ni kuielezea miradi mbalimbali inayotekelezwa ikiwa ni muendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Maji iliyoanza machi 16,2024 na kilele chake ni machi 22,2024.Aidha Afisa Uhusiano wa Mamlaka ameipongeza serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuelekeza fedha nyingi kwenye miradi ya maji ukiwemo mradi mkubwa wa Kiwira utakaogharimu…

Read More

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wafanyabiashara kumi kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu. Akitoa taarifa Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watu kumi wanahusishwa na tukio hilo Ilomba Jijini Mbeya. KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHAB Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wafanyabiashara kumi kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu. Akitoa taarifa Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watu kumi wanahusishwa na tukio hilo Ilomba Jijini…

Read More