Author: Mbeya Yetu

Rais Mstsaafu wa Awamu ya Nne na Mjumbe Maalum wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kiongozi wa Burkina Faso Kepteni Ibrahim Traore mjini Ouagadougou na kushuhudiwa na baadhi ya maafisa waandamizi wa nchi zote mbili. Mhe. Kikwete aliwasilisha pia salamu za Rais Samia ambazo zilielezea umuhimu wa nchi za Afrika kuimarisha ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kama njia muhimu kwa bara hilo kujitegemea, hususan katika kipindi hiki ambapo misaada kutoka nchi za magharibi imepungua kwa kiasi kikubwa.

Read More

Mbeya, Tanzania – Aprili 2025
Wakazi wa maeneo ya Mwansekwa na Igodima jijini Mbeya wameeleza furaha yao kufuatia kuboreshwa kwa huduma ya upatikanaji wa maji safi katika maeneo yao, hali ambayo ni tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

Wananchi hao wameipongeza Serikali pamoja na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA-UWSA) kwa juhudi walizozifanya kuhakikisha wanapata huduma ya maji kwa uhakika. Wamesema kuwa huduma hiyo imeleta unafuu mkubwa katika maisha yao ya kila siku, hasa kwa upande wa wanawake na watoto waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta maji.

“Kwa sasa tunapata maji karibu kabisa na nyumbani, tofauti na zamani tulipokuwa tukiteseka,” alisema mmoja wa wakazi wa Mwansekwa.

Kwa upande wake, MBEYA-UWSA imeeleza kuwa maboresho hayo ni sehemu ya mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kuboresha huduma za maji mijini na vijijini kwa kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanapata huduma hiyo muhimu kwa maendeleo na ustawi wa jamii.

Read More

Pembenzoni mwa Mkutano wa Uongozi wa Afrika wa nane jijini Kampala Uganda leo, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa kama mjumbe maalum, amewasilisha ujumbe maalum kwa Rais Yoweri Kaguta Museveni kutoka kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan. Rais Museveni alimshukuru kwa ziara na kumuomba amfikishie salamu zake kwa Mheshimiwa Rais Samia na watu wa Tanzania.

Read More

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameongoza waombolezaji kutoka Kundi la Afrika pamoja na mataifa rafiki ya Afrika ndani ya IPU kutoa salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge la Zambia, Mhe. Nelly Mutti, kufuatia kifo cha Katibu wa Bunge la Zambia, Marehemu Roy Ngulube, aliyefariki dunia tarehe 7 Aprili 2025 nchini Uzbekistan. Tukio hilo limefanyika leo, tarehe 8 Aprili 2025, jijini Tashkent, Uzbekistan.

Read More

Watumishi wa Afya ambao ni Mabalozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kutoka Dodoma jana wamefanya ziara ya mfano kuitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma (DRRH) na kutoa msaada wa vifaa tiba na dawa kwa watoto wanaohitaji huduma za afya. Akizingumza na Wafanyakazi wa wodi ya Watoto wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Bi. Naima Mkingule ambae ni Kiongozi wa msafara amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za afya, jamii, na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma bora na kwa haraka.”Katika kuhakikisha watoto wetu wanapata huduma bora za afya, ni muhimu kuunganisha nguvu zetu. Ushirikiano…

Read More