Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wafanyabiashara kumi kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu. Akitoa taarifa Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watu kumi wanahusishwa na tukio hilo Ilomba Jijini Mbeya. KUMI WAKAMATWA WAKITOROSHA KILO 9.5 ZA DHAHAB
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia wafanyabiashara kumi kwa tuhuma za kutorosha kilo 9.5 za madini ya dhahabu.
Akitoa taarifa Waziri wa madini Anthony Mavunde amesema thamani ya dhahabu iliyokamatwa ina thamani ya shilingi bilioni 1.5 ambapo watu kumi wanahusishwa na tukio hilo Ilomba Jijini Mbeya.
Mavunde amesema tukio hili ni la pili kutokea Mkoani Mbeya na kuagiza kamishina wa madini kuzifuta leseni zote zinazomilikwa na watu hao pamoja na leseni zote zinazomilikea na watu hao nje ya Mkoa wa Mbeya
Sanjari na kukamatwa watu hao na dhahabu hiyo pia vimekamatwa vifaa vya kuchomea dhahabu na mizani ya kupimia pamoja na dawa za kusafishia uchunguzi ukikamilika watafikishwa mahakamani
Aidha Mavunde ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa watu wanaomiliki maeneo bila kuyafanyia kazi