Maadhimisho ya siku ya usikivu Duniani yameadhimishwa Kitaifa Mkoani Mbeya mgeni rasmi akiwa ni Waziri wa Afya Ummy Mwalimu aliyewakilishwa na Dkt Maisara Karume maadhimisho yalifofanyika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Katika hotuba yake Dkt Maisara Karume amesema takwimu za kitaifa zinaonesha kuwa tatizo la usikivu ni kubwa na baadhi ya mikoa wanawake wanaongoza kwa tatizo la usikivu.
Dkt Maisara ameagiza hospitali zote za Rufaa za mikoa nchini kuwa na vifaa kwa ajili kubaini changamoto ya usikivu kwa wananchi.
Rais wa Jumuia ya Wataalamu wa masikio,pua na koo Tanzania Dkt Edwin Liyombo ameishukuru serikali kwa kuongeza wataalamu na vifaa katika hospitali nyingi nchini.
Naye Amina Mfaki mwakilishi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI amesema serikali inaendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga hospitali sanjari na kutoa elimu kwenye jamili ili kupunguza tatizo la usikivu kwa wananchi.
Taarifa imesomwa na Raphael Gabriel Katibu wa Jumuia ya wataalamu wa masikio pua na koo ikionesha Jumuia ina wataalamu zaidi ya mia moja ishirini wa kada mbalimbsli ambao walihusika kutoa huduma za afya,uchunguzi na utabibu katika wiki ya maadhimisho.
Dkt Benedict Ngunyale ni Daktari Bingwa hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya mkuu wa kiitengo cha masikio,pua na koo amesema katika wiki ya maadhimisho wamezifikia shule kumi na moja za msingi na zaidi ya wanafunzi elfu tatu wamepatiwa elimu na uchunguzi wa masikio na matibabu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya Dkt
Godlove Mbwanji amesema changamoto nyingi za usikivu zinasababishwa na upigaji wa muziki kwa sauti ya juu mathalani kwenye huduma za vinyozi ambazo huathiri pia wateja.
Mwinyi Kondo kutoka Wizara ya Afya ameomba vyombo vya habari kutoa nafasi kwa waataalamu kutoa elimu kwenye jamii.
Kupitia maadhimisho haya mbali ya wananchi kunufaika na elimu kutoka kwa wataalamu wa wananchi wamefanyiwa uchunguzi na kupatiwa matibabu bure.