Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amekabidhi msaada wa nondo zaidi ya hamsini kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Mbalizi Road Jijini Mbeya.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mbalizi Road Mheshimiwa Adam Simbaya amesema Mheshimiwa Mahundi aliombwa kuchangia nondo thelathini lakini yeye ametoa nondo hamsini ikiwa ni zaidi ya kiwango kilichoombwa.“Hii itakuwa ofisi ya mfano nchini kutokana na ubora wa ujenzi unaoendelea ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mbeya Patrick Mwalunenge la kuzitaka Kata zote Mkoa wa Mbeya kuwa na ofisi za kisasa”alisema Simbaya.
Mahandisi Maryprisca Mahundi amekuwa akichangia shughuli mbalimbali za ujenzi wa ofisi za Chama Cha Mapinduzi kama UWT,Vijana na Jumuia ya Wazazi sanjari na kuwawezesha Wanawake kiuchumi kwa kuwagawia mitaji bure pamoja na majiko ya gesi na mitungi yake.
Mahundi amekuwa akiishi na kauli mbiu ya Taasisi ya ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF)”Twende Tukue Pamoja”