Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti ya PAPU, mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) unaofanyika Makao Makuu ya Ofisi za Umoja huo Jijini Arusha leo tarehe 11 Juni, 2024.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU), mara baada ya kufungua rasmi Baraza hilo linalofanyika Makao Makuu ya Ofisi za Umoja huo Jijini Arusha leo tarehe 11 Juni, 2024.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Wawakilishi wa Wizara za Kisekta kutoka nchi Wanachama wa Umoja wa Posta Afrika (PAPU), mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la Umoja wa Posta Afrika (PAPU) unaofanyika Makao Makuu ya Ofisi za Umoja huo Jijini Arusha leo tarehe 11 Juni, 2024.
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) na viongozi Wakuu wa Umoja wa Posta Afrika na wawakilishi wa Umoja wa Posta Duniani (UPU), wakati wa kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania na wa Afrika kabla ya kufungua rasmi Mkutano wa 42 wa Baraza la Utawala la (PAPU) unaofanyika Makao Makuu ya Umoja huo Jijini Arusha leo tarehe 11 Juni, 2024.
Mkutano huo unaofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 11 hadi 12 Juni, 2024 ukiwa na lengo la kujadili maazimio na taarifa za vikao vya Kamati za Wataalam wa masuala ya posta vilivyofanyika tarahe 03 hadi 07 Juni, 2024 ambapo yalijadiliwa masuala mbalimbali yanayohusu Fedha na Utawala, Sera na Kanuni, Uendeshaji na Teknolojia pamoja na Mkakati.
Mkutano huu umehudhuriwa na wajumbe kutoka nchi wanachama wa PAPU pamoja na wadau mbalimbali wa Sekta ya Posta kutoka barani Afrika na wajumbe wa Sekretarieti ya Umoja wa Posta Duniani.