Mamlaka ya Bima Tanzania TIRA imemtembelea manusura wa ajali ya gari iliyosababisha vifo vya watu nane katika eneo la Igodima Jijini Mbeya hivi karibuni.
Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya ambako anatibiwa.abiria wenzie nane kati ya tisa waliokuwa katika gari hilo wamefariki dunia katika ajali hiyo.