Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYAUWSA)imeandaa maadhimisho ya huduma kwa wateja yanayofanyika oktoba 7,2024 hadi oktoba 11,2024 yenye lengo la kuenzi huduma zinazotolewa na Mamlaka sanjari na wanayopata wateja wao.
CPA Gilbert Kayange amesema hitaji la upatikanaji wa maji Jijini Mbeya na Mbalizi ni lita 90m wakati upatikanaji wa maji kwa sasa ni 72.5m kwa siku.
Aidha amesema Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira imetoa ofa kwa wadaiwa wote waliokatiwa maji kuanzia oktoba mosi hadi oktoba 30 watapaswa kulipa nusu ya deni Ili kurejeshewa huduma ya maji.
Pamoja na utaratibu huo Kayange amesema Mamlaka itatoa elimu kwa wateja wao ili wajue haki zao pia wajibu wao.