Bilioni 5.3 kujenga soko la Kimataifa la ndizi Kiwira Rungwe
Jumla ya shilingi bilioni 5.3 kujenga soko la Kimataifa la ndizi eneo la Kalasha Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Hayo yameelezwa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda katika mkutano Maalumu na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Kata ya Katumba.
Mwakagenda amesema kuanzishwa kwa soko hilo mbali ya kuongeza kipato kwa Halmashauri kutanufaisha pia wakulima wa ndizi ambao watanufaika na bei nzuri kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi.
Baadhi ya wakulima wa zao la ndizi wameomba kuharakishwa kwa mchakato wa ujenzi ili bidhaa zao zipate bei nzuri sanjari na kuwaondolea kadhia ya kuuzia ndizi kwenye tope.