Matukio mbalimbali katika picha Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi aalipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) leo Julai 16, 2024 jijini Dar es Salaam. Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akioneshwa namna Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ikifanya ufuatiliaji wa maudhui ya watoa huduma wa sekta ya utangazaji alipotembelea makao makuu ya Mamlaka hiyo leo Julai 16, 2024 jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akimsikiliza Dkt. Jabiri Kuwe, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania akimfafanulia namna Mamlaka hiyo inavyotoa huduma kwa watoa huduma na walaji wa huduma za mawasiliano wakati wa ziara yake ya kikazi katika Mamlaka hiyo iliyofanyika leo Julai 16, 2024 jijini Dar es SalaamNaibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi akipitishwa katika gari lenye teknolojia ya kupima masafa na ubora wa mawasiliano walipotembelea makao makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ajili ya kupitishwa kwenye majukumu yanayotekelezwana Mamlaka hiyo leo Julai 16, 2024 jijini Dar es Salaam
Na Faraja Mpina, WHMTH, Dar es Salaam
NAIBU Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa ubunifu na ufanisi katika usimamizi na utatuzi wa changamoto na malalamiko katika sekta ya Habari na Mawasiliano.
Mhandisi Mahundi ametoa pongezi hizo leo Julai 16, 2024 alipotembelea Mamlaka hiyo kwa ajili ya kupitishwa kwenye majukumu yanayotekelezwa na mamlaka hiyo na namna wanavyoshughulikia masuala ya habari na mawasiliano yaliyo chini ya dhamana yao.
Ameongeza kuwa kufanya vizuri kwa Mamlaka hiyo kunaisaidia Wizara lakini pia inaongeza imani ya wananchi kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika ziara hiyo, Mhandisi Mahundi amejionea namna mamlaka hiyo inavyohudumia wateja; teknolojia wanazotumia kupima masafa na ubora wa mawasiliano; na ufuatiliaji wa maudhui ya watoa huduma za mawasiliano
Akizungumzia kuhusu kukua kwa teknolojia ya Habari na Mawasiliano Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt. Jabir Kuwe amesema matumizi ya teknolojia hiyo yana fursa nyingi za kidijiti lakini pia yana changamoto zake.
Akifafanua hilo ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuwa makini katika matumizi ya teknolojia hiyo na kile wanachochapisha mtandaoni kwasababu kupitia teknolojia taarifa nyingi binafsi huvunwa na kuchakatwa wakati mwingine bila ya mhusika kujua kuwa ameacha alama.
Mhe. Mhandisi Mahundi anafanya ziara ya kikazi ya kutembelea taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo pamoja na makampuni yanayotoa huduma za mawasiliano kwa lengo la kufahamu majukumu wanayotekeleza na namna wanavyowahudumia wateja wao na wananchi kwa ujumla.