IiNaibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amekutana na kuzungumza na ujumbe wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran 14 Juni, 2024 katika Ofisi za Wizara, Mji wa Serikali – Mtumba, Dodoma.Ujumbe huo umeongozwa na Mshauri wa Kimkakati wa Waziri wa Wizara hiyo, Bw. Hossein Mirzapoor pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kimataifa na Maendeleo ya Uuzaji Bidhaa Nje wa Wizara hiyo, Bw. Ali Saneian.
Katika kikao hicho, wamejadili masuala mbalimbali ya kuongeza mashirikiano katika Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
#SmartTanzania #TzyaKidijitali #KaziIendelee