Utalii wa kiutamaduni katika kikundi cha Maasai Boma katika kijiji cha Mikumi
Wananchi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa na Nyererevinanufaika na Mradi wa REGROW unaotekelezwa nchinikupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.
Hayo yamesemwa Jijini Mbeya na Bi. Blanka Aquilinus Tengia Naibu Msimamizi wa Mradi wa REGROW unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na TANAPA, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) na Bodi ya Bonge la Maji Rufiji (RBWB).Lengo la mradi ni kuboresha usimamizi wa maliasili sanjari na kukuza utalii Kusini mwa Tanzania.
Blanka Tengia amesema mradi ulianza mwaka 2017 baada ya tafiti mbalimbali kufanyika na ni wa thamani ya Dola za marekani milioni 150 sawa na takribani shilingi za kitanzania bilioni 345.
Aidha, moja ya shughuli zinazotekelezwa ni kuboresha miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege na majengo ndani ya hifadhi nne za kipaumbele. na miundombinu ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Kiwanja cha ndege Kiganga – Ruaha
Blanka amesema kipaumbele cha kwanza ni kuboresha miundombinu ya barabara, Viwanja vya ndege na miundombinu ya maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji.
Kikundi cha Watu na Mazingira Mkata, Ufugaji wa kuku
Mbali ya kuboresha miundombinu Mradi wa REGROW unachochea ukuaji wa wa wananchi kiuchumi hususani wanaoishi nyirani na hifadhi zilizotajwakwa kusaidia uanzishwaji wa miradimiradi mbalimbali ya kujikwamua kiuchumi, ufadhili wa masomo kwa vijana, vikundi kupewa mtaji wa kukopeshana kwa riba nafuu na kuiwezesha jamii kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu. Pia mradi unatekeleza shughuli za utunzaji wa vyanzo vya maji kwenye eneo la juu la Hifadhi ya Taifa Ruaha ambavyo ni vyanzo vya maji kwa mto Ruaha Mkuu.
Katika hatua nyingine Blanka amesihi wananchi wanaoishi pembezeno mwa hifadhi kuzipenda na kuzitunza hifadhi hizo na kufanya Utalii wa ndani ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kukuza Utalii kupitia filamu ya The Royal Tour.
Malazi kwa Madereva waongoza watalii – Ruaha
Kiwanja cha Ndege Mtemere – Nyerere
Naye Sharif Abdul Afisa Mwandamizi kitengo cha mahusiano Jamii na ujirani mwema hifadhi ya Taifa Ruaha amesema kupitia mradi wa REGROW wameandaa Muongozo rafiki wa kupokea na kushughulikia malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka hifadhi.
Amesema kupitia mradi wa REGROW viongozi na kamati za kushughulikia malalamiko kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka mkoa wamejengewa uwezo kwa kupewa elimu namna ya kutumia muongozo huo ili kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi. Lengo nikuhakikisha wananchi wanaoathirika na shughuli za hifadhi au Mradi wa REGROW wanawasilisha malalamiko yao na yanashughulikiwa kwa utaratibu unaofahamika.
Hatua ya pili lalamiko litafanyiwa uchambuzi Ili kubaini iwapo linahusiana na masuala ya mradi au hifadhi kisha kuelekezwa katika idara au kamati husika na kipaumbele kitatolewa kwa kuzingatia aina ya malalamiko.
Aidha Abdul amewasihi wananchi wenye malalamiko wafike ofisi za Serikali ya Kijiji nakuwasilisha malalamiko yao au wapige simu ya bure moja kwa moja kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha namba 0800110801 na Wizara ya Maliasili na Utalii namba 0800110804 endapo lalamiko linahusu Hifadhi au Mradi wa REGROW. Malalamiko yote yatashughulikiwa kwa usiri na mlalamikaji atalindwa na sheria na tararibu za nchi.