Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust ametoa futari kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.Katika hafla hiyo Dkt Tulia Ackson amewakilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera ambaye amesema Dkt Tulia amefanya mengi kwa Jiji la Mbeya ikiwemo vifaa vya ujenzi kwa shule mbalimbali sanjari na kutoa bima za afya kwa wazee zaidi ya elfu sita.Shekhe wa Mkoa wa Mbeya Msafiri Ayasi Njalambaha amesema Dkt Tulia Ackson amekuwa akisaidia jamii bila kujali itikadi zao kama kuwasaidia vifaa vya shule wanafunzi wenye uhitaji na ujenzi wa nyumba.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Mbeya Parick Mwalunenge ni miongoni mwa watu walioshiriki futari hiyo amesema Dkt Tulia anakiwakilisha vema Chama Cha Mapinduzi na Jimbo la Mbeya akiwa Bungeni.Naye MNEC Ndele Mwaselela amepata fursa ya kutoa neno akiwataka Wanachama cha Mapinduzi kuweka ulinzi kwa Dkt Tulia ili aendelee kutekeleza majukumu ya Kitaifa.