Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele,
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na wahariri wa vyombo vya
Habari kuhusu maandalizi ya Uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
uliofanyika leo tarehe 12 Juni, 2024 mkoani Dar es Salaam.

*****
Na. Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
imewaasa wahariri wa vyombo vya habari kuwahabarisha na kuwaelimisha wananchi
juu ya umuhimu wa kujiandikisha na kuboresha taarifa zao kwenye Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura.

Akizungumza wakati wa kufungua mkutano
wa Tume na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 12
Juni, 2024, Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs
Mwambegele amesisitiza juu ya umuhimu wa vyombo vya habari na nafasi yao katika
kuhakikisha kwamba wananchi wanapata taarifa sahihi na kwa wakati.
Mkutano huo ambao ni mwendelezo wa
mfululizo wa vikao vya wadau vilivyoanza tarehe 07 Juni, 2024 ulikuwa na lengo
la kuwapa wadau hao wa uchaguzi taarifa mbalimbali za maandalizi kwa ajili ya
kuanza rasmi kwa zoezi la uboreshaji wa Daftari.
“Tume inatarajia kupata ushirikiano
mkubwa zaidi kutoka kwenu, kwa kuwafikishia wananchi taarifa sahihi na kwa
wakati zinazohusu zoezi lililopo mbele yetu la uboreshaji wa Daftari la Kudumu
la Wapiga Kura na kuwahamasisha wananchi wenye sifa ya kujiandikisha kuwa
wapiga kura, wajitokeze kwa wingi kwa tarehe ambazo Tume imeziweka kwa kila
kituo,” amesema Jaji Mwambegele.
Amewashukuru wahariri hao kwa kuwa kwa
nyakati tofauti wamekuwa wakitoa fursa kwa Tume kutumia vipindi vya redio na
televisheni kutoa elimu ya mpiga kura ikiwa ni pamoja na kutoa fursa ya
kuchapisha habari na makala kwenye magazeti za kutoa elimu na kufafanua hoja
mbalimbali zinazotolewa na wadau wa uchaguzi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi
wa Tume, Bw. Kailima, R. K ameviasa vyombo vya habari kuelimisha wananchi
kuzingatia sheria, kanuni, miongozo, taratibu na maelekezo yanayohusu uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura badala ya kulalamika.
“Kupitia vyombo vya habari tuwashauri wote watakaodhani
kuna changamoto kutumia njia zilizopo kwenye sheria, kanuni, miongozo, taratibu
na maelekezo yanayohusu uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura badala
ya kuanza kulalamika,” amesema.
Sehemu ya Wahariri wa
Vyombo vya Habari wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa Tumen a wahariri hao
kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura uliofanyika leo tarehe 12 Juni, 2024 mkoani
Dar es Salaam.

Wajumbe wa Tume wakiwa katika mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele,
akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Tume na wahariri wa vyombo vya
Habari kuhusu maandalizi ya Uboreshaji
wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura
uliofanyika leo tarehe 12 Juni, 2024 mkoani Dar es Salaam. Kulia ni Mjumbe wa Tume, Mhe. Jaji Asina Omari na Katikati ni Makamu Mwenyekiti
wa Tume, Mhe. Jaji wa Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk.

Picha za pamoja baina ya meza kuu na washiriki wa Mkutano huo.