Mkaguzi kata ya Lwenzera Wilaya ya Geita Mkoani Geita amewataka Walimu Wa Shule ya Sekondari Bugando Kufuata Maadili ya Kazi huku akiwataka kutambua kuwa Jamii inawategemea katika kuwafundisha na kutoa malezi Mema kwa Wanafunzi.
Hayo yamebainishwa na Mkaguzi wa Kata hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi A/INSP Pili Kulele wakati alipotembelea Shule hiyo ambapo amewaomba walimu kujikita katika kuwafundisha wanafunzi na kutoa malezi mema ili wawe msaada katika Jamii na kata hiyo kwa ujumla.
Mkaguzi kulele amewasihi walimu hao na kuwaambia kuwa kumekuwepo na baadhi ya walimu wasiofuata maadili ya kazi hiyo na kuchafua taswira nzuri na historia nzuri iliyowekwa na kada hiyo katika ufundishaji na kutoa wataalam wa kada mbalimbali akiwemo mkaguzi huyo.
Vile vile amewakumbusha walimu hao kutambua kuwa ualimu ni wito ambapo amebainisha kuwa hatopenda kusikia katika kata yake kuna changamoto ya kimaadili kwa baadhi ya walimu.
Sambamba hilo amewambia kuwa zipo club za kielimu katika shule ambapo amesisitiza zitumike kukumbushana mambo muhimu na kushauriana kitaaluma.