WANANCHI MBEYA WALIA KUVAMIWA NA TAZARA
Wakazi wa Iyunga,Ivumwe,ltuha,ltezi na Nsalaga Jijini Mbeya wameiomba Serikali kutolea ufafanuzi mgogoro wa ardhi baina yao na Shirika la Reli Tanzania na Zambia(TAZARA)baada ya Shirika hilo kuweka mawe(Bicons)katika maeneo yao sanjari na kuwataka wabomoe nyumba zao zinazodaiwa kuwepo mita hamsini ndani ya hifadhi ya reli kinyume na makubaliano.
Wananchi hao kwa nyakati tofauti wakiwa na nyaraka mbalimbali kuhusiana na mgogoro huo wamepaza sauti zao baada ya kugonga ukuta ofisi zote ikiwemo TAZARA na ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya.