Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewaagiza Mawaziri wanaohusika na utatuzi wa migogoro ya mipaka ikiwemo sekta za Ardhi, mifugo na Maliasili kwenda wilayani Mbarali mkoani Mbeya kushughulikia mgogoro unaodaiwa kuibuka hivi karibuni.
Waziri Mkuu Majaliwa ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Mbarali Francis Mtega kutoa hoja kulitaka bunge kujadili kwa dharula mgogoro kwa taarifa kuwa mmoja wa wafugaji mifugo yake inashikiliwa na amedhamiria kujinyonga na hadi alipowasilisha hoja hiyo alikuwa bado anadhibitiwa na wananchi wanzake asitimize azma hiyo kwa sababu ya mifugo yake kukamatwa na kushikiliwa.
Akitoa majibu ya serikali kufuatia hoja hiyo Waziri Mkuu amewataka Mawaziri wote wa kisekta kwenda kutatua mgogoro huo haraka na kuwasilisha taarifa kamili ofisini kwake kesho saa mbili usiku.