Zaidi ya bilioni kumi na Moja zimetumika kukamilisha ujenzi wa miradi mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ndani ya miaka mitatu tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassani kuapishwa kuwa Rais wa awamu ya sita kutokana na aliekuwa rais wa awamu ya Tano kufariki Dunia mwanzoni mwa mwaka 2022 Hayati Dkt.Pombe Joseph Magufuri.
Hayo yamebainishwa na Mganga mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya Dkt.Abdallah Mmbaga wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya hali ilivyo tangu Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwepo madarakani.
Baadhi ya wananchi waliopo Mkoani Mbeya wamezungumzia hali ya huduma ilivyo katika hospitali hiyo wakisema maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali yamefanya hospitali hiyo kuwa kimbilio la haraka kwao huku wakiwapongeza watumishi wa hospitali hiyo kuwa na lugha nzuri kwa wagonjwa tofauti na zamani.
Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya huhudumia wakazi wa Wilaya za Mbeya,Kyela,Chunya,Mbarali na Rungwe.