Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa kushirikiana na Taasisi ya 1 New Heart Tanzania inayojihusisha na upimaji wa moyo kwa watoto imewaka kambi ya siku tatu ya uchunguzi na upimaji wa moyo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 kwa wakazi wa Nyanda za Juu Kusini.
Akiongea wakati wa zoezi hilo Dkt. Nuru Mniwa Mkuu wa Idara ya Watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema lengo la kambi hiyo ya siku tatu ni kutoa huduma ya uchunguzi na vipimo kwa watoto chini ya umri wa miaka 14 ili kutambua matatizo mbalimbali ya moyo yanayowakumba pamoja na kuwapuguzia gharama za kusafiri umbali mrefu kwenda kupata huduma hiyo.
“..changamoto kubwa ni uwezekano wa watoto hawa kufika Taasisi ya Moyo ya JKCI pale wanapobainika na tatizo la moyo kutokana na umbali na gharama za kujikimu”.- Dkt. Nuru Mniwa
Kwa upande wake Dkt. Gloria Mbwile, Daktari Bingwa Mbobezi wa magonjwa ya Moyo kwa watoto Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya amesema, magonjwa ya moyo kwa watoto yamegawanyika katika makundi mawili ikwemo magonjwa ya kuzaliwa nayo pamoja na yale yanayoytokana na maambukizi.