Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujidhatiti katika utangazaji utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Utalii nchini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameyasema hayo leo Machi 17,2024 wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya TTB jijini Dar es Salaam .
TTB YATAKIWA KUJIDHATITI UTANGAZAJI UTALII NCHINI
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii imeitaka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kujidhatiti katika utangazaji utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na Utalii nchini.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Timotheo Mnzava (Mb) ameyasema hayo leo Machi 17,2024 wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Ofisi za Makao Makuu ya TTB jijini Dar es Salaam .
” Tunawapongeza kwa kazi nzuri na kuwatia moyo muendelee kuifanya kazi mliyokasimiwa kwa weledi kwa manufaa ya Taifa letu” Mhe. Mnzava amesema.
Aidha, wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wameitaka TTB kupanua wigo wa utangazaji utalii kwa kutangaza maeneo mapya ambayo hayajafikiwa.
Pia, wameitaka TTB kuwa na mpango wa urithishanaji madaraka kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi.
Naye, Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amekiri kufanyia kazi mapendekezo ya kamati hiyo ili kuikuza Sekta ya Maliasili na Utalii.
Ziara hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania, Dkt.Ramadhan Dau pamoja na Menejimenti ya Bodi ya Utalii Tanzania.