Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Mbeya Mjini, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 20 Disemba, 2024 ametoa msaada wa vyakula na mboga kwa Wananchi wa Mbeya Mjini wanaoishi katika mazingira magumu Jijini Mbeya ambapo kwa siku ya leo ametembelea Kata 9 na kuwafikia Wananchi 1030 ambapo lengo kuu ni kuwafikia watu wengi wenye uhitaji katika Kata zote 36 za Jiji hilo.
Akitoa msaada huo, Dkt. Tulia amesema kuwa, lengo kuu la kufanya hivyo ni kufikisha tabasamu kwa Wananchi wake ambao hawajiwezi ili wafurahie katika msimu huu wa sikukuu za Chrismass na Mwaka mpya.