Tarehe 27.11.2024 saa 12:30 jioni eneo la Mbembela Jijini Mbeya katika
barabara kuu ya Mbeya – Tunduma, Gari lori namba T.537 DNC na Tela
namba T.241 ARG aina FAW iliyokuwa imepakia madini ya Sulphur ikitokea
Dar es Salaam kuelekea Tunduma Mkoa wa Songwe ilipoteza uelekeo na
kugonga magari sita, bajaji nne, Pikipiki moja na kusababisha vifo vya watu
watatu, wawili papo hapo na mmoja amefariki dunia leo Novemba 28, 2024
akiwa anaendelea na matibabu.
Magari yaliyohusika katika ajali hiyo ni T.199 DYF Toyota Coaster, SU 44682
Toyota Double Cabin mali ya Shirika la Posta Mbeya iliyokuwa ikiendeshwa na
Fredy Mwasanga [48] mkazi wa Soweto, Gari T.134 DXK Toyota Double Cabin
iliyokuwa ikiendeshwa na Lusekelo Mwaseba [48] mkazi wa Sae, Gari T.370
ABN Toyota Land Cruiser, Gari T.344 BTS Toyota Cresta na Gari T.474
EHL/t.449 EHL aina ya FAW iliyokuwa ikiendeshwa na Alon Ruben [50] mkazi
wa Isanga.
Aidha, katika ajali hiyo Bajaji nne ziligongwa ambazo ni MC.446 DYK, MC.649
DWL, MC.138 DKC na MC.261 EBN na Pikipiki moja ambayo haijafahamika
namba zake za usajili. Waliofariki katika ajali hiyo bado hawajatambulika,
wawili jinsia ya kiume na mmoja jinsia ya kike. Majeruhi tisa wanaendelea na
matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva kushindwa kulimudu Gari kwenye
eneo lenye mteremko. Jitihada za kumtafuta Dereva kwa kushirikiana na
mmiliki wa Gari zinaendelea.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea kutoa wito kwa madereva kuwa
makini na kufuata sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza
kuepukika.
Imetolewa na:
Benjamin Kuzaga – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.
Trending
- KOCHA MEXIME AAHIDI KUREJESHA FURAHA KWA MASHABIKI MBEYA CITY FC, KUSHUSHA ”VIFAA” DIRISHA DOGO
- *DKT. MWIGULU AMBANA MKANDARASI UJENZI WA BARABARA YA KITAI-RUANDA*
- MBEYA UWSA YAONGEZA UFANISI, NAIBU WAZIRI WA MAJI AZINDUA MAGARI YA KISASA
- Kila mwanamke mzuri alimuacha kabla ya kupata msaada huu
- Naibu Waziri wa Maji Mathew: Aweka Mkazo Kwenye Miradi ya Maji Mbeya na Chunya
- Hafla ya Makabidhiano ya Vitabu vya Fidia vya Mradi wa Chanzo cha Mto Kiwira
- WAKUTUBI WAKUTANA MBEYA WAJADILI MFUMO BORA WA MAKTABA NA USOMAJI VITABU KIDIJITALI
- MKUU WA MKOA WA MBEYA BENNO MALISA AHIMIZA MATUMIZI YA TEKNOLOJIA KULINDA FEDHA ZA UMMA

