Kuelekea Kilele cha siku ya maadhimisho ya Tiba ya magonjwa ya Dharura, wataalamu wa Afya kutoka Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya leo tarehe 24 mei, 2024 wamekutana na kikosi cha Jeshi la zimamoto na uokoaji, Madereva Bajaji na Bodaboda lengo ikiwa ni kutoa elimu juu ya kukabiliana na wagonjwa wa dharura wawapo katika maeneo yao ya kazi.
Akiongea kwa niaba na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya, Mkurugenzi wa Tiba hospitalini hapa Dkt. Uwesu Mchepange amesema makundi hayo waliyoyachagua ni muhimu sana kwa kuwa hospitali ni kituo cha mwisho cha kupokea wagonjwa wa dharura hivyo ni vema kupeleka elimu pia kwa makundi ambayo yanahusika kwa mara ya kwanza pindi mgonjwa anapopata dharura.