Watumishi wa Afya ambao ni Mabalozi wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kutoka Dodoma jana wamefanya ziara ya mfano kuitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Dodoma (DRRH) na kutoa msaada wa vifaa tiba na dawa kwa watoto wanaohitaji huduma za afya.
Akizingumza na Wafanyakazi wa wodi ya Watoto wa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, Bi. Naima Mkingule ambae ni Kiongozi wa msafara amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya taasisi za afya, jamii, na wadau mbalimbali ili kuhakikisha kuwa watoto wanapata huduma bora na kwa haraka.
“Katika kuhakikisha watoto wetu wanapata huduma bora za afya, ni muhimu kuunganisha nguvu zetu. Ushirikiano kati ya taasisi za afya, jamii, na wadau wengine ni msingi wa mafanikio yetu katika kutatua changamoto za kiafya zinazowakabili watoto.” – Bi. Naima Mkingule, Kiongozi wa Msafara.
Mkingule ameeleza kuwa msaada huo wa vifaa tiba na dawa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Wizara ya Afya katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za afya maeneo mbalimbali nchini, hususan kwa watoto, ambao wanahitaji huduma za matibabu ili kuweza kupona magonjwa yanayoathiri maisha yao.
Trending
- MADEREVA BODABODA MKOANI IRINGA WALAANI VITENDO VYA UVUNJIFU WA AMANI.
- MAHAFALI YA 23 YA TAASISI YA UHASIBU TIA KAMPASI YA MBEYA, RC MALISA AWAALIKA WAWEKEZAJI MKOANI MBEYA.
- Ilinde biashara dhidi ya husda na mikosi
- Fanya hivi kuvutia fursa mpya za kazi
- WASHINDI WA MAWAZO BUNIFU WANAZUONI TAASISI YA UHASIBIU TIA KUFANYA ZIARA YA KIMAFUNZO NJE YA NCHI
- “KUNUNA MWISHO – MWALUNENGE AWAPA MOTISHA VIJANA WA KIWIRA: PESA IPO, CHANGAMKIA FURSA”
- Alivyovutia fursa kubwa katika kutengeneza samani na kuuza
- MEYA ISSA ACHARUKA—AMLIPUA MKANDARASI WA SOKO MATOLA NA STENDI KUU KWA KUCHELEWESHA UJENZI

