Bi. Betty(Rehema) Fwelefwele Kalala wa Musoma vijijini mkoa wa Mara anamtafuta baba yake mzazi aitwae METHOD KAPINGA kabila Mnyakyusa dini Muislamu anatokea mkoa wa Mbeya. Pia hata familia ya mzee huyo kama atakuwa amefariki.
Mzee method kwa sasa umri wake utakuwa kuzidi miaka 75 kama atakuwa bado yupo hai. Mzee Method alimwacha mtoto wake toka akiwa na miezi 3 kuzaliwa.
Wajihi wake.
Alikuwa na chongo jicho moja na alikuwa anavaa miwani
Historia kwa ufupi.Mama wa betty
Mama wa Betty anaitwa SARA FWELEFWELE KALALA (yupo hai) alikutana na Method kijijini Butiama mkoa wa Mara mwaka 1976. Bi Sara alikuwa anafanya kazi kwa mdogo wa mwalimu Nyerere aitwae Joseph Nyerere. Na Method alikuwa ni mwalimu mkuu shule ya msingi Butiama. Bi sara alikuwa akiishi kwa kaka yake aitwae Juma Fwelefwele Kalala.
Waliingia kwenye mahusiano na ndipo walipopata mtoto wa kike mwaka 1977 ambapo baba mtu alipendekeza jina la Rehema ambalo ni jina la shangazi yake.
Baada ya bi Sara kujifungua alirudi kijijini kwao Nyasembe-Majita bay-Musoma vijijini. Baada ya miezi mitatu bwana Method akaenda kumwona mtoto na mama yake akiwa amembata na marafiki zake wawili ambao walikuwa wanafanya kazi wote shule ya msingi butiama mwanzoni ila waliamishiwa shule ya msingi Murangi ambayo ipo karibu na kijiji cha nyasembe huku Method akibaki butiama hivyo bwana Method alitoka butiama na kuwapitia marafiki zake hapo.
Marafiki hao ni:-
Monika Madaha baada ya kustaafu alirudi butiama.
Ally Adieli baada ya kustaafu alirudi Tanga
Christina.
Walipofika kwao. Bwana Method alitaka kulipa faini na kumchumbia Sara kisha arudi nae butiama pamoja na mtoto wao. Bahati mbaya wazazi wa Sara walikataa.
Bwana Method aliondoka kurudi butiama na baada ya muda aliamishiwa shule ya msingi Kiabatari na toka hapo hawakuonana tena.
Baada ya kuona kimya Rehema alibadilishwa jina na kuitwa Betty na kupewa ubini wa mama yake.
Kwa sasa Betty ana umri wa miaka 47 ameolewa na ana watoto. Anaishi kijiji cha Chumwi na mamanyake yupo palepale Nyasembe.
Namba za simu za Betty:-
+255 766 465 950
Namba za watoto wa Betty:-
George
+255 766 865 738
+255 621 881 206
Paul
+255 693 034 975
Mama wa Betty
+255 756 819764
+255 688 044 974
Mdogo wa betty
Mariam]
+255 768 832 370
+255 787 137 835
Hivyo kulingana na maelezo hayo. Yeyote atakayemfahamu au kuijua familia ya mzee buyo awasiliane na namba hizo hapo juu.