#mbeyayetutv
Wakili Msomi na Kada wa Chama Cha Mapinduzi CCM Kapteni Sambwee Shitambala Mwalyego amejitokeza kuchukua fomu kuwania Ubunge Jimbo la Mbeya mjini.
Shitambala amesema ameguswa kuwania nafasi hiyo akitumia haki yake ya msingi, akidhamiria kuendeleza pale alipoishia Spika wa Bunge Dkt Tulia Ackson ambaye amehamia kuwania katika jimbo jipya la Uyole.