Ibada ya Jumapili katika kanisa moja maarufu eneo la Kihonda ilikatizwa ghafla kwa taharuki, baada ya mwanamke mmoja kuvamia madhabahu akiwa na machozi na kuanza kupiga kelele akimtuhumu mume wake, ambaye ndiye mchungaji wa kanisa hilo, kwa usaliti wa ndoa yao.
Kwa mujibu wa waumini waliokuwepo, ibada ilikuwa ikiendelea kwa hali ya utulivu hadi pale mwanamke huyo alivyoingia ghafla kupitia mlango wa upande wa madhabahu akiwa amevaa vazi la kawaida na viatu vya mpira. Bila kutoa ishara yoyote ya kusalimia, alianza kulia kwa sauti na kumwita mchungaji huyo kwa jina lake la nyumbani, jambo ambalo liliwashangaza wengi.
“Mwanzo tulidhani ni muumini aliyekuwa na shida ya kiroho,” alisema dada mmoja wa kanisa hilo. “Lakini tuliposikia maneno yake, tukagundua ni mke wa mchungaji.”
Mke huyo alimshtaki hadharani mumewe kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa muumini mmoja anayehudhuria kanisa hilo. Kilichowashangaza wengi hata zaidi ni hatua ya mchungaji huyo kuangusha Biblia yake na kutokomea kwa kasi kupitia mlango wa nyuma bila hata neno moja. Soma zaidi hapa