Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya Kata jijini Mbeya wametakiwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya uchaguzi ili kuepusha vurugu wakati wa mchakato wa uchaguzi mkuu.
Tahadhari hiyo imetolewa na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Jimbo, Anamary Joseph, anayesimamia majimbo ya Mbeya Mjini na Uyole, wakati wa mafunzo kwa wasimamizi wa uchaguzi wa kata hizo.
Afisa Uchaguzi wa Jiji la Mbeya, Gregory Emmanuel, amesisitiza umuhimu wa wasimamizi hao kuwa na nyaraka muhimu kama Katiba na kanuni za uchaguzi ili kusimamia kikamilifu utoaji na urejeshaji wa fomu za wagombea pamoja na ratiba ya kampeni.
Washiriki wa mafunzo hayo wameonesha utayari wao kutekeleza majukumu kwa weledi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu