Ilikuwa ni siku ya kawaida sokoni Morogoro, watu wakihangaika na shughuli zao, baadhi wakipiga kelele kuuza bidhaa huku wengine wakinunua. Lakini ghafla, kelele nyingine zilianza kuvuma sio za biashara, bali za mkurupuko wa kiakili kutoka kwa kijana mmoja aliyekuwa akipiga makelele huku akirandaranda katikati ya soko bila viatu, akisema maneno ya ajabu.
“Nilikunywa chai ya mapenzi! Namsahau hata mama yangu! Nani alinifanyia hivi?” Alilia kwa sauti kubwa akijiinamia huku macho yakiwa mekundu kwa hasira na uchungu. Watu walimzingira, wengine wakidhani amepagawa au ni mlevi, lakini maneno yake yalizidi kuwachanganya watu: “Chai ile ilikua tamu, lakini sasa naishi kwa ndoto! Nilimwambia kila kitu hata password ya mama yangu!”
Majirani na wafanyabiashara waliomfahamu walishangaa kwani kijana huyo, aitwaye Selemani, alikuwa ni fundi maarufu wa simu na alijulikana kwa utulivu wake. Hakuwa mlevi wala mhuni, lakini siku hiyo alionekana kama mtu aliyepoteza mwelekeo kabisa. Soma zaidi hapa