Ni tukio la kushangaza lililoshuhudiwa katika kanisa moja la kifahari jijini Arusha, ambapo harusi iliyotarajiwa kuwa ya kifalme iligeuka kuwa sinema ya kutisha mbele ya wageni waliokuwa wamefurika kushuhudia. Jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Gerald, alipigwa na kifafa dakika chache tu baada ya kusema wazi kwamba hatambui wala hataki kumhusisha bibi yake wa kwanza kwenye maisha yake mapya ya ndoa.
Sherehe hiyo ilikuwa imepangwa kwa miezi mingi. Gerald, ambaye ni mfanyabiashara maarufu mkoani Arusha, alikuwa ameandaa harusi ya kukata na shoka na mwanadada mrembo mwenye jina la ushawishi mtandaoni.
Hata hivyo, wengi walishangazwa kuwa hakukuwa na dalili zozote za heshima wala ushirikishwaji wa bibi yake wa kwanza, ambaye walifunga ndoa naye miaka minane iliyopita na kuzaa naye watoto wawili.
Kama ilivyo kawaida, mchungaji aliuliza maswali ya kawaida kabla ya kufungisha ndoa. Lakini kabla hata ya kuendelea mbele, Gerald alisimama ghafla na kusema kwa sauti ya dharau: “Naomba ieleweke mbele za Mungu, mimi sina mke mwingine. Ndoa ya zamani ilikua ya kiholela, na sipo tayari kuitambua.” Soma zaidi hapa