Jesca alikuwa binti mzuri mwenye heshima na tabasamu la kuvutia, mzaliwa wa Mwanza. Tangu akiwa mdogo, ndoto yake kubwa ilikuwa kuanzisha familia yenye furaha – kuwa na mume mwenye mapenzi ya dhati na watoto ambao wangeikamilisha furaha yake. Lakini kadri miaka ilivyozidi kusonga, ndoto hiyo ilianza kumponyoka taratibu.
Wakati marafiki zake wa karibu wakiolewa mmoja baada ya mwingine, Jesca alibaki akiwa shahidi wa furaha yao bila yeye mwenyewe kuonja ladha ya ndoa. Alipofikisha miaka 27, watu wa karibu na hata familia yake walimwona bado ana nafasi kubwa ya kuolewa. Lakini alipovuka miaka 30, shinikizo likazidi. Mama yake mara kwa mara alimwambia: “Jesca mwanangu, mbona muda unazidi kusonga? Hivi unategemea nini tena?”
Jesca alijaribu mara kadhaa kuingia kwenye mahusiano. Alikutana na wanaume wengi – baadhi walionekana wazuri mwanzoni lakini waligeuka kuwa wachepukaji; wengine walikuwa hawana dhamira ya kuoa, bali walitaka starehe tu. Wengine walimkatisha tamaa kwa kumwambia wazi kuwa hakuwa mke wa ndoto zao. Alilia machozi mengi usiku akiwa kitandani, akijiuliza kwa nini bahati ya mapenzi ilikuwa ikimkwepa.
Miaka ikazidi kusonga, Jesca sasa akiwa na miaka 34, alihisi moyo wake umechoka. Wakati fulani aliwaza kuachana kabisa na ndoto ya kuwa mke na mama, na badala yake aelekeze nguvu zake zote kwenye biashara ndogo aliyokuwa ameianzisha. Lakini moyoni, alijua bado anatamani kushirikiana maisha na mtu wa kumpenda na kumheshimu. Soma zaidi hapa