Kijana machachari, Dulla alizaliwa katika kijiji kidogo nje ya mji wa Tabora, eneo lililojulikana kwa mashamba ya tumbaku, misitu ya miombo na utamaduni wa watu wenye upendo na mshikamano. Alikuwa kijana mchapakazi na mwenye heshima, lakini safari yake ya kupata mwenzi wa maisha haikuwa rahisi kama ya vijana wengine.
Katika ukoo wao kulikuwepo na imani za kale—vifungo vya kiukoo vilivyoaminika kuvuruga mambo ya ndoa kwa baadhi ya wanaume. Wazee wa ukoo walizungumza kimya kimya kuwa wanaume wachache walishawahi kupata shida hiyo, lakini hakuna aliyewahi kudhani kuwa Dulla angekuwa mmoja wao.
Miaka ilivyopita, Dulla alijitahidi kujenga maisha yake. Alianza shughuli ya useremala na kwa bidii yake alianza kujulikana kijijini kama fundi mwenye mikono ya dhahabu. Alijenga nyumba ndogo, akaanza kupiga hatua kimapato, na kila mtu aliamini muda si mrefu angeleta mke nyumbani. Lakini mambo hayakuwa rahisi kama walivyotarajia.
Kila alipojaribu kuanzisha mahusiano, jambo fulani la ajabu lilikuwa likivuruga. Mara msichana atatoweka bila sababu, mara wazazi watakataa, mara mambo yatakwenda kombo ghafla. Mwishowe akina mama wa kijijini wakaanza kunong’ona, “Huyu kijana ana mkosi wa kifamilia.”
Dulla alianza kuamini maneno hayo polepole. Hakuonyesha sana, lakini moyoni alihisi uzito. Kwa miaka mingi aliendelea kufanya kazi zake akiwa kimya, akiepuka hata mazungumzo ya mahusiano kwa sababu alichoka kuumia. Soma zaidi hapa

