Kama vijana wengi wa rika lake, Mpoki kutoka Bukoba, mji uliopo kando ya Ziwa Victoria, alikuwa shabiki mkubwa wa soka, hasa Ligi Kuu Italia (Serie A), na alijihusisha kwa kiasi kikubwa na mchezo wa kubashiri matokeo ya michezo, maarufu kama betting.
Kwa miaka mingi, Mpoki aliwekeza pesa zake kidogo kidogo alizopata kwa kufanya vibarua, akitarajia siku moja atapata ushindi mkubwa utakaomtoa kwenye umasikini. Lakini bahati haikuwa upande wake. Alikuwa akikaribia sana kushinda; mara kwa mara, ubashiri wake ulipata mechi zote isipokuwa moja tu ndiyo iliharibu tiketi yake, na kumuacha akipoteza pesa zake.
Alijaribu mikakati yote—kubashiri timu ndogo, kubashiri timu kubwa, kucheza Odds za chini, kucheza Odds za juu—lakini mwisho wa siku, alibaki na mfuko tupu.
Hali ya maisha ilianza kuwa ngumu sana kwa Mpoki. Familia yake ilikuwa ikimtegemea, na matumaini yake ya kubadilisha maisha yake yalikuwa yakififia.
Aliamini kabisa kuwa kuna kitu kilikuwa kinamzuia kupata ushindi huo mkubwa, kama vile amefungwa kwa bahati mbaya.
Siku moja, akiwa ameketi kwenye duka la betting akilaumi mchezo wa Fiorentina uliomharibia tiketi nyingine, alikutana na rafiki yake wa zamani, Bw. Hassan. Hassan aliona huzuni usoni mwa Mpoki na akamuuliza kinachomsumbua. Soma zaidi hapa

