Mbunge wa Jimbo la Uyole, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson (@tulia.ackson), ameendelea kutoa sadaka kwa familia zisizo na uwezo katika kipindi cha kuelekea sikukuu ya Krismasi kwa kutoa chakula na fedha.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Dkt. Tulia amesema ushirikiano mzuri kati ya viongozi wa mitaa na wananchi ndiyo umefanikisha kuwatambua walengwa sahihi, akibainisha kuwa leo ilikuwa zamu ya Kata ya Ilemi, ambapo kaya 13 zimenufaika, huku jumla ya kaya 130 zikitarajiwa kupata msaada huo katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Uyole.
Ameongeza kuwa zoezi hilo ni endelevu na litaendelea katika kata nyingine kadri ratiba itakavyoruhusu, kwa lengo la kuwafikia wananchi wenye uhitaji mkubwa zaidi.

