Author: Mbeya Yetu

Rais wa Mabunge Duniani Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson ametokeza kujiandikisha katika daftari la wapiga kura Mtaa wa Uzunguni A kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika novemba 27 mwaka huu.

Dkt Tulia Ackson amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutoa hamasa kubwa watu kujiandikisha ambapo mpaka sasa uandikishaji umefikia asilimia 83.

Amewataka wananchi ambao hawajajiandikisha watumie muda uliobaki kujiandikisha katika Mitaa yao.

Read More

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani  amejiandikisha kwenye daftari la wakazi katika mtaa wa Chimuli II kwenye kituo cha Shule ya Msingi Chadulu jijini Dodoma leo Oktoba 19, 2024.   Akizungumza baada ya kujiandikisha, Bw. Kailima aliwasisitiza wananchi umuhimu wa kujitokeza kwa wingi kuandikishwa katika maeneo yao ili watimize haki yao ya kikatiba ya kupiga kura.   “Nimetoka kujiandikisha katika orodha ya wakazi ambayo itazaa daftarinla orodha ya wapiga kura kwaajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa, niwaombe na kuwasihi wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na…

Read More

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amefungua rasmi Kongamano la nne la Afrika la Uhifadhi wa Biolojia lililowakutanisha wataalamu wabobezi takribani 300 kutoka nchi mbalimbali Barani Afrika na nje ya Bara la Afrika lengo ikiwa ni kuendeleza uhifadhi wa maliasili na Bioanuwai. Ufunguzi huo umefanyika katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka (College of African Wildlife Management- CAWM), Moshi Mkoani Kilimanjaro leo Oktoba 19,2024. “Tunahitaji uhifadhi endelevu kwa faida ya kizazi cha sasa na baadaye kwani uhifadhi ni ajira, unaongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla kutokana na mapato na kuingiza fedha…

Read More

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema Mbio za Kimataifa za Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni chachu katika kukuza utalii na kuiweka Tanzania katika ramani ya riadha na utalii Kimataifa. Mhe.Chana ametoa kauli hiyo usiku wa Oktoba 18,2024 wakati wa hafla ya kuzindua mbio za 23 za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon 2025 jijini Dar es Salaam. “Mbio hizi za Kimataifa zenye washiriki zaidi ya 12,000 na wasindikizaji wao kutoka nchi zaidi ya 56 zimekuwa na manufaa makubwa kwetu, hasa katika kukuza utalii kwa kupitia michezo yaani sports tourism na kukuza uchumi” amesisitiza Mhe. Chana.…

Read More

Wanariadha wa Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi waliofanya vyema katika mashindano ya Mbio ndefu na fupi katika michuano ya mbio maarufu NAGAI City Marathon 2024 wamepongezwa kwa kuibuka washindi wa kwanza na kupewa medali za dhahabu. Pongezi hizo zimetolewa na Afisa Mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Debora Lukololo kwa Niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, wakati wa mapokezi ya wachezaji hao waliowasili Nchini leo Oktoba 18, 2024 kupitia Uwanja wa Kimataifa wa Ndege (KIA). Mbio hizo zilifanyika jijini Nagai nchini Japan Oktoba 13, 2024 huku Wanamichezo hao wakipeperusha vyema Bendera ya…

Read More

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Alhaj Dkt Abubakar Zubeiry bin Ali amehimiza wananchi nchini kote kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Wapiga Kura la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili waweze kutimiza haki yao kikatiba ya kuwachagua viongozi wanaowataka wa Serikali za Mitaa katika maeneo wanapoishi. Mufti na Sheikh Mkuu ametoa wito huo leo mara baada ya kushiriki katika zoezi la uandikishwaji kwenye daftari hilo katika mtaa wa Kwamndolwa, kata ya Kwamndolwa katika wilaya ya Korogwe mkoani Tanga. Amewataka vijana na watu wazima, wake kwa waume wafanye juu chini watumie hizi siku tatu zilizosalia kwenda vituoni na kujiandikisha…

Read More

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima Ramadhani akifafanua jambo wakati wa mafunzo ya siku moja kuhusu sharia za uchaguzi kwa Maafisa Wakuu wa Upelelezi wa Wilaya nchini. Mafunzo hayo yamefanyika leo Oktoba 17, 2024 jijini Dodoma. Pamoja nae ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini DCI Ramadhani Kingai.  ***** Na Mwandishi wetu, Dodoma Maafisa wa Polisi nchini wametakiwa kujenga  tabia ya kujikumbusha sheria mbalimbali ikiwemo zinazohusu masuala ya uchaguzi ili kuepuka kuyumbishwa na wanasiasa wanaoamua kupotosha yaliyomo katika sheria hizo kwa maslahi yao binafsi. Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume…

Read More