Author: Mbeya Yetu

UMWAGAJI ZEGE UJENZI WA BANIO MRADI MTO KIWIRA WAANZA

Miradi wa Maji mto Kiwira unaendelea kwa ufanisi mkubwa kama ilivyokusudiwa na kasi ikielekezwa kwenye umwagaji wa zege kwenye banio utakaodumu kwa saa thelathini na sita unaofanywa na kampuni ya China Railway Construction Group ambapo awali ilifanyika kazi ya kuchepusha mto.

Hayo yamebainishwa na Mhandisi Barnabas Konga Mkurugenzi wa masuala ya Ufundi Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYAUWSA) ambaye pia ni Msimamizi wa mradi wa Maji mto Kiwira.

Konga amesema shughuli ya zege itafanyika usiku na mchana ili ifikapo mwezi machi mwakani mradi uwe umekamilika.

Aidha Konga amempongeza Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson kwa ufuatiliaji wa pesa za mradi sanjari na kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa pesa za utekelezaji wa mradi.

Konga amesema vijiji vya Unyamwanga, Mbeya 1 na Swaya vinavyopitiwa na mradi huo vitanufaika na huduma ya maji.

Robert Mkasela kutoka kampuni ya GKW anayemsimamia mkandarasi amesema mradi unasimamiwa kwa ubora, usalama na wakati uliokusudiwa.

Kwa upande wake Wang Yang mkandarasi wa mradi huo amesema mradi utakamilika kama ilivyokusudiwa lengo ni kukamilisha banio na tanki la kupokelea maji kabla ya msimu wa mvua kuanza.

Read More

Mwenyekiti wa Tume, Mhe. Jaji (Rufaa) Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa uchaguzi uliofanyika leo Julai 8,2024 mkoani Tabarea. Washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo. Washiriki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Kailima, R. K akiwasilisha mada kuhusu maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza kwa wadau wa Mkoa wa Tabora.  Mkurugenzi wa Idara ya Daftari na TEHAMA wa Tume, Stanslaus Mwita akiwasilisha mada ya mfumo. …

Read More

Tanzania ni miongoni mwa nchi zitakazo nufaika na mradi wa Sustainable Ocean Phase II”unaosimamiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Haki za Binadamu nchini Denmark(Danish Institute of Human Rights). Hayo yamebainishwa na Mshauri Mkuu wa Taasisi hiyo Bi.Carol Rask wakati walipotembelea Ofisi ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora hivi karibuni Jijini Dodoma. Bi.Carol alisema mradi huo unaotarajiwa kutaekelezwa kwa muda wa miaka minne unafadhiliwa na SIDA. mradi huo umelenga kuimarisha ulinzi wa mazingira kwa wavuvi wadogo na jamii zinazowazungukaalisema Bi.Carol Aidha Bi Carol alisema katika kutekeleza mradi huo wamefanya ziara nchini Tanzania iliyolenga kutafuta wadau mbalimbali ambapo moja…

Read More

Bilioni 5.3 kujenga soko la Kimataifa la ndizi Kiwira Rungwe

Jumla ya shilingi bilioni 5.3 kujenga soko la Kimataifa la ndizi eneo la Kalasha Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Hayo yameelezwa na Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Rungwe Gabriel Mwakagenda katika mkutano Maalumu na Waandishi wa Habari uliofanyika katika Kata ya Katumba.

Mwakagenda amesema kuanzishwa kwa soko hilo mbali ya kuongeza kipato kwa Halmashauri kutanufaisha pia wakulima wa ndizi ambao watanufaika na bei nzuri kwa wanunuzi kutoka nje ya nchi.

Baadhi ya wakulima wa zao la ndizi wameomba kuharakishwa kwa mchakato wa ujenzi ili bidhaa zao zipate bei nzuri sanjari na kuwaondolea kadhia ya kuuzia ndizi kwenye tope.

Read More

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (COSEA SINKALA, MBEYA.CM) Wilaya ya Mbeya vijijini Akimu Sebastian Mwalupindi amemtaka Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Njeza kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi kwa maslahi ya wananchi badala ya kusikia maneno ya watu juu ya watu wanaojipitisha jimboni kutaka ubunge mwakani 2025 kitendo anachosema ni kinyume na taratibu za CCM. Mwalupindi amesema hayo wakati akizungumza kwenye mkutano wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Mbeya vijijini uliofanyika katika mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya. Amesema wanaojipitisha kabla ya muda watashughulikiwa kwani kuna vyombo husika vinavyoona kwakuwa Chama Cha Mapinduzi…

Read More

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Dkt Michael Battle akitoa hotuba yake kwa Kiswahili jana jioni katika hafla ya kuadhimisha siku ya Uhuru wa Marekani maarufu kama Julai 4, katika makazi yake Oysterbay jijini Dar es salaam.

Julai 4 ndio siku kuu ya nchini Marekani, ikiadhimisha kupitishwa kwa Tamko la Uhuru mnamo Julai 4, 1776 na Rais Thomas Jefferson, alipottangaza kupatikana kwa uhuru wa koloni kumi na tatu za Marekani kutoka utawala wa Uingereza.

Umuhimu wa Julai 4 kwa Wamarekani unatokana na sababu kadhaa kuu. Katika siku hii, Kongresi yao ilipitisha rasmi Tamko la Uhuru, ambalo lilielezea matamanio ya koloni kuunda taifa tofauti lililo huru kutoka utawala wa Uingereza.

Tamko hilo la Uhuru lilikuwa alama ya uhuru kamili na demokrasia. Liliainisha misingi ya msingi ya uhuru, usawa, na kutafuta furaha, ambayo ina maana kubwa kwa maadili ya Marekani.

Kupitishwa kwa Tamko kuliweka msingi wa Vita vya Mapinduzi, hatimaye kupelekea kuanzishwa kwa Marekani kama taifa huru. Ushindi katika vita na mkataba wa amani uliofuata na Uingereza ulithibitisha Julai 4 kama tarehe muhimu katika historia ya Marekani.

Kwa Wamarekaniu, kuadhimisha siku ya Uhuru Julai 4 kumekuwa jadi ya muda mrefu, ikitia nguvu umoja wa kitaifa na uzalendo.

Siku hiyo huadhimishwa na sherehe mbalimbali, ikiwemo fataki, gwaride, matamasha, na mikusanyiko ya familia, ambayo huleta watu pamoja kusherehekea urithi wao wa pamoja.

Ingawa tarehe nyingine, kama vile kusainiwa kwa Katiba au kumalizika kwa Vita vya Mapinduzi, pia ni muhimu, Julai 4 ina umuhimu wa kipekee wakati ambapo koloni za Marekani zilichukua msimamo thabiti kwa uhuru wao. Siku hii tangu hapo imekuwa sikukuu ya kitaifa inayoheshimu misingi ya nchi na roho ya kudumu ya watu wake.

Read More