Author: Mbeya Yetu

Na Mwandishi Wet MKESHA mkubwa wa kuvuka nusu mwaka Kufanyika Dodoma Juni 5 ndani ya Ukumbi wa Jakaya Conversion Center Mkesha huo unaenda kwa jina la ACROSS THE YEAR umeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Emanuel Shemdoe chini ya huduma ya LOVE OF CHRIST na waombaji wa kila mwezi Jijini Dodoma. “Huu ni mkesha mkubwa unao hudhuriwa na watu wa dini zote bila kubagua” Alisema mwalimu Shemdoe Waimbaji mbalimbali watahudumu katika mkesha huo. Waimbaji hao ni pamoja na Waimbaji – KKKT Arusha Road Praise team, Cathedral Worship team, Essence of Worship,Agape Gospel Band, Pamoja na John Lisu, Sax tulivu…

Read More

Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi Wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson imetoa Miche 1120 ya Parachichi kwa Wananchi wa Kata Kumi na Tatu (13) Mbeya Mjini.

Miche hiyo ya Parachichi imetolewa bure kwa lengo la kuhamasisha Wananchi utunzaji wa Mazingira kwa kupanda Miti Yenye faida zaidi ya Moja ili kujiongezea kipato kupitia zao la Parachichi.

Kata zilizo nufaika ni Pamoja na Iganjo, Iduda, Igawilo, Nsalaga, Itezi, Isyesye, Ilomba, Mwakibete, Tembela, Mwasanga, Iyela, Sinde na Iganzo ikiwa ni awamu ya Tatu baada ya awamu ya Kwanza kutoa Miche zaidi ya 1000, zoezi hili ni endelevu na litazifikia kata zote za Mbeya Mjini.

Read More

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Cde: Juma Z. Homera amemuagiza Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamini Kuzaga kumsaka na kumkamata Kijana anayepatikana Ntokela Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya Kwa Kosa la Kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Maneno Makali na Kisha kuichoma moto Picha inayomuonyesha Mh:Rais.

RC Homera amelaani vikali Kitendo hicho kuwa si Cha Maadili Wala Uungwana na Kiko tofauti na Utamaduni halisi wa Wananchi Mkoani Mbeya.

Hata hivyo ametoa Masaa 24 kwa Kamanda Kuzaga Kumkamata Kijana huyo ili alisaidie Jeshi la Polisi juu ya tuhuma hizo na Mashambulizi hayo ambayo kayaelekeza Moja kwa Moja kwa Mh: Rais Dkt: Samia Suluhu Hassan.

Mwisho RC Homera amewasihi Wananchi Mkoani Mbeya kutojiingiza kwenye Vitendo viovu kwa Kukashifu Viongozi Makusudi badala yake wajikite katika Utafutaji na Uchapa Kazi kwa Manufaa ya Familia zao na Tanzania kwa Ujumla.

Read More

ASANTE MBEYA YAGUSA WAHITAJI IGURUSI MBARALI YATOA MAGODORO 46 KWA WAHITAJI.

Umoja wa Asante Mbeya Project unaoongozwa na Mkurugenzi wake Daniel Mwanakatwe(MC DANNY FM)umetoa magodoro arobaini na sita yenye thamani ya shilingi milioni mbili laki tano na elfu thelathini kwa watu wanaoshi mazingira hatarishi Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya hafla iliyofanyika Kijiji cha Lunwa Kata ya Igurusi Mgeni rasmi akiwa ni Mheshimiwa Diwani Hawa Kihwele.

Daniel Mwanakatwe ambaye ni Mkurugenzi wa Umoja huo amesema umoja wao una malengo matatu la kwanza kuwagusa Wahitaji pili kusaidiana wao na tatu kuwezeshana kiuchumi na kupeana fursa.

Amesema lengo la kutoa magodoro ni kuungana na Serikali kwa lengo la kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia unaofanywa na ndugu wa karibu pindi wanapowatembelea katika kaya zao.

“Godoro hili litamsaidia mtoto pindi wanapokuja wageni mtoto hatalala na ndugu badala yake mtoto atahamishwa peke yake ili mgeni alale peke yake lengo si kuvunja undugu bali ni kuweka ulinzi kwa watoto”alisema Mwanakatwe.

Mlezi wa Umoja huo Tumaini Mbembela ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za injili na mjumbe wa mkutano Mkuu Taifa kupitia Umoja wa Wanawake Mkoa wa Songwe amesema tendo lililofanyika ni sadaka mbele za Mungu.

Aidha Mbembela amewataka wadau wengine kuungana na Asante Mbeya ili kuwasaidia wahitaji kwani ni wengi.

Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Igurusi Hawa Kihwele ameupongeza uongozi wa Asante Mbeya kwa ubunifu mkubwa wa kuwagusa wahitaji kwenye Kata yake.

Casmiri Pius ni Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Igurusi amesema msaada umekuja kwa wakati kwani wahitaji ni wengi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lunwa Isihaka Kimamule ameshukuru umoja wa Asante Mbeya kuwasaidia wananchi wake kwani wahitaji ni wengi.

Maclina Michael mkazi wa Lwanyo amesema yeye ni mmoja wa watu wanaoshi mazingira hatarishi amesema godoro alilopewa litaisadia familia yake.

Esther Mwaifuge Mkazi wa Chamoto amewashukuru wana Umoja wa Asante Mbeya kwa kuwajali watu wenye uhitaji.

Saita Mwanyingili bibi mwenye umri wa miaka tisini naye hakusita kuwashukuru wana Umoja wa Asante Mbeya kwa kuwafikiria watu wenye uhitaji kama yeye.

Lwitiko Minga amesema amesema binafsi asingeweza kununua godoro kutokana uchumi wake kuwa duni.

Umoja wa Asante Mbeya una wanachama nchi nzima na wanamiliki usafiri wao wa basi aina ya Coaster na wapo mbioni kununua usafiri mwingine ili kupanua wigo wa huduma na kuongeza kipato.

Read More