Author: Mbeya Yetu

Kambi ya macho maalum kwa ajili ya wagonjwa wa mtoto wa jicho iliyofanyika Hospitali ya Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imepata mafanikio makubwa kwa wagonjwa waliofika Hospitalini hapo kuipongeza serikali na Shirika la Hellen Keller International kufanikisha matibabu bure. John Mpozayo(73) mkazi wa Saza Wilaya ya Songwe Mkoa wa Songwe ni mmoja wa watu waliokuwa wanasumbuliwa na mtoto wa jicho kwa macho yote mawili kwa miaka mitano naye hakusita kufika Hospitalini hapo ili kupatiwa matibabu. Amesema alikuwa akipata changamoto mbalimbali kutokana na kadhia ya kutoona kwani mara nyingine alishindwa kwenda Kanisani na maeneo mengine hata kwenda maliwato alikuwa akiongozwa na…

Read More

Anastazia Timotheo Kasela (26) mkazi wa Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya ni mwanamke aliyezaliwa na ulemavu wa macho amelishukuru Shirika la Hellen Keller International kwa kufanikisha matibabu ya mtoto wa jicho yaliyofanyika Hospitali ya Wilaya ya Chunya. Anastazia aliyejaliwa kuwa na familia ya watoto wawili hakuwahi kuwatambua kwa sura zao wala hajui sura ya mumewe bali aliweza kuitambua sauti yake tu. Katika Kambi hiyo ya mtoto wa jicho iliyoanza juni 19,2024 na kutamatika juni 24,2024 Anastazia ni miongoni mwa wagonjwa waliofika Hospitalini hapo akiwa hana matumaini lakini siku moja baada ya kufanyiwa upasuaji na kufunguliwa macho alijikuta mwenye furaha…

Read More

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Kigoma leo tarehe 22 Juni, 2024 kuhusiana na kusogezwa mbele kwa uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo sasa utafanyika tarehe 20 Julai, 2024 mkoani Kigoma.  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza na waandishi wa Habari mkoani Kigoma leo tarehe 22 Juni, 2024 kuhusiana na kusogezwa mbele kwa uzinduzi wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambapo sasa utafanyika tarehe 20 Julai,…

Read More