Author: Mbeya Yetu

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYAUWSA)imeandaa maadhimisho ya huduma kwa wateja yanayofanyika oktoba 7,2024 hadi oktoba 11,2024 yenye lengo la kuenzi huduma zinazotolewa na Mamlaka sanjari na wanayopata wateja wao.

CPA Gilbert Kayange amesema hitaji la upatikanaji wa maji Jijini Mbeya na Mbalizi ni lita 90m wakati upatikanaji wa maji kwa sasa ni 72.5m kwa siku.

Aidha amesema Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira imetoa ofa kwa wadaiwa wote waliokatiwa maji kuanzia oktoba mosi hadi oktoba 30 watapaswa kulipa nusu ya deni Ili kurejeshewa huduma ya maji.

Pamoja na utaratibu huo Kayange amesema Mamlaka itatoa elimu kwa wateja wao ili wajue haki zao pia wajibu wao.

Read More

  Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (Mstaafu) Mbarouk Salim Mbarouk leo tarehe 04 Oktoba, 2024 ametembelea na kuzungumza na washiriki wa mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki katika Wilaya ya Wete na Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba yanayofanyika kwa siku mbili. Mafunzo hayo yanafanyika ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa sita wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ambao utajumuisha mikoa mitano ya Zanzibar. Uboreshaji wa Daftari kwenye maeneo hayo utaanza Oktoba 07 hadi Oktoba 13, 2024 na vituo vitakuwa vinafunguliwa kuanzia saa 2:00 asubuhi na kufungwa saa…

Read More

Mjumbe wa Tuhe Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Balozi Omar Ramadhan Mapuri akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili ya watendaji wa Uboreshaji ngazi ya majimbo katika mikoa yote ya Kisiwa cha Pemba, Zanzibar. Mafunzo hayo yamefungwa leo Oktoba o2, 2024 amewataka watendaji wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  Visiwani Zanzibar kuzingatia Katiba ya nchi, sheria za Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani na kanuni zake katika utekelezaji wa majukumu yao. Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Mstaafu Mbarouk Salim Mbarouk (katikati) akiwa meza kuu na…

Read More

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mhe. Ester Mahame, ametembelea kambi ya matibabu inayotolewa na Madaktari Bingwa na Bobezi wa Rais Samia Suluhu Hassan katika hospitali ya wilaya ya Vwawa kwa lengo la kujionea hali ya utoaji huduma pamoja na kuonge na kuwafariji wagonjwa waliojitokeza kupatiwa matibabu katika kambi hiyo, ambayo itakaa mkoani Songwe kwa siku 7. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Mahame amesisitiza umuhimu wa maboresho wakubwa ya huduma za afya nchini yakiyofanyika na kumpongeza Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani na Serikali ya awamu ya sita kwa kuweka mazingira mazuri ambayo yanawawezesha…

Read More