Author: Mbeya Yetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisherehekea Siku ya Mtoto wa Afrika akiwa pamoja na wajukuu, Ikulu jijini Dar es Salaam. Siku hii huadhimishwa Juni 16 ya kila mwaka. Katika kuadhimisha siku hii, Rais Samia amesisitiza umuhimu wa Serikali, familia na jamii kushirikiana kuhakikisha watoto wanapata malezi bora yenye maadili mema, na kuhakikisha usalama wa mtoto ni jukumu la jamii nzima na siyo mzazi tu, vilevile kuwapatia elimu na historia za kuwahimiza uzalendo kwa nchi yao tangu wakiwa wadogo.

Read More

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Taifa wa Bingu uliopo Lilongwe nchini Malawi kushiriki Mazishi ya Kitaifa ya aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Malawi Hayati Dkt. Saulos Chilima leo tarehe 16 Juni 2024. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Malawi Mhe. Agnes Kayola na Kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akimfariji Rais wa Jamhuri ya Malawi Mhe. Dkt. Lazarus Chakwera mara baada ya kuwasili…

Read More

IiNaibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) amekutana na kuzungumza na ujumbe wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran 14 Juni, 2024 katika Ofisi za Wizara, Mji wa Serikali – Mtumba, Dodoma.Ujumbe huo umeongozwa na Mshauri wa Kimkakati wa Waziri wa Wizara hiyo, Bw. Hossein Mirzapoor pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Masuala ya Kimataifa na Maendeleo ya Uuzaji Bidhaa Nje wa Wizara hiyo, Bw. Ali Saneian. Katika kikao hicho, wamejadili masuala mbalimbali ya kuongeza mashirikiano katika Sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA). #SmartTanzania #TzyaKidijitali…

Read More