Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
- Yamenifika makubwa baada ya kuikataa mimba yake
- Happy birthday Dr. Tulia
- Viongozi 11 wa CHADEMA washikiliwa na Polisi Mkoa wa Songwe
- ZIARA YA NAIBU WAZIRI MAHUNDI ZANZIBAR
- Jinsi ya Kufikisha Malalamiko Kuhusu Mradi wa REGROW na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha
- Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi Akagua Hali ya Mawasiliano Kisiwani Kojani, Pemba
- Inauma sana: Mtoto wangu kaenda chuo kikukuu katumbukia katika umalaya na dawa za kulevya
- WALIOKUWA WANAENDA KUMZIKA NEEMA ALIYEFIA KARIAKOO WAPATA AJALI, MMOJA AJARIKI
Author: Mbeya Yetu
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imekuwa inafanya kazi na benki ya Citibank ya Marekani kwa zaidi ya miaka 35 na imekuwa ikipokea ushauri wa mambo ya kifedha kupitia Benki Kuu ya Tanznaia (BoT). Amesema hayo jana (Jumanne, Septemba 24, 2024) mara baada ya kukutana na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki hiyo, Bw. John Dugan, kwenye makao makuu ya benki hiyo, jijini New York, Marekani. “Serikali ya Tanzania inaishukuru sana Benki ya Citibank kwa kuwa imeshiriki katika ujenzi wa uchumi ikiwemo na upatikanaji wa fedha za mikopo, kuishauri Serikali katik amasuala ya fedha na kufadhili miradi mikubwa inayoendelea kujengwa nchini,”…
Ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya itakayogharimu zaidi ya shilingi milioni sabini unaenda kwa kasi.
Nyumba hiyo inajengwa kwa hisani ya Taasisi ya Maryprisca Women Empowerment Foundation (MWEF) inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Mbeya Edina Mwaigomole pamoja na Lucia Sule Katibu wa UWT Mkoa wa Mbeya wamewaongoza Wenyeviti na Makatibu wa UWT Mkoa kutembelea na kuona maendeleo ya ujenzi huo ambapo wamepongeza juhudi zinazofanywa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Nyumba hiyo iliyonza kujengwa wiki moja iliyopita inatarajiwa kumalizika mwezi disemba mwaka huu ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda la kuzitaka Wilaya na Mikoa yote nchini kujenga nyumba za Makatibu.
REGROW ni Mradi wa Serikali unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa Lengo la kuboresha usimamizi wa maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na hifadhi ya Mikumi, Udzungwa na Nyerere wanatekeleza mradi huu. Kutokana na utekelezaji wa mradi wa REGROW au shughuli za Hifadhi ya Taifa Ruaha, unaweza kuwa na maoni au malalamiko yanayotokana na shughuli hizo. Kila mtu ana nafasi ya kutoa malalamiko yake kuhusu changamoto zinazotokana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na shughuli za Mradi wa REGROW. Iwe malalamiko ya athari zinazotokana na usimamizi wa hifadhi, kero za ardhi, unyanyasaji na…
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb), ametaja mambo makubwa aliyoyafanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha Sekta ya Maliasili na Utalii. Ameyasema hayo leo Septemba 24, 2024 alipokuwa akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Peramiho, Mkoani Ruvuma. Mhe. Chana amesema kuwa Rais ameifungua dunia kwa kutangaza vivutio vya utalii vilivyoko nchini Tanzania kupitia filamu yake ya “Tanzania the Royal Tour “ sambamba na kuielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kufungua Utalii Kusini. Ametumia fursa hiyo kuwahamasisha Watanzania kuitazama filamu hiyo na kutembelea vivutio mbalimbali vya…
UMOJA WA MABUNGE DUNIANI WAJIHAKIKISHIA USHIRIKIANO ENDELEVU NA UMOJA WA MATAIFA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amethibitisha kuwa ushirikiano endelevu baina ya Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Umoja wa Mataifa (UN) ni wa muhimu katika kutekeleza ajenda mbalimbali za pamoja kwa manufaa ya dunia.
Dkt. Tulia alitoa kauli hiyo tarehe 23 Septemba, 2024, alipokuwa akiwasilisha hotuba kwa niaba ya IPU katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliojadili mustakabali wa dunia kwa siku zijazo (Summit of the Future), uliofanyika katika Ofisi za UN jijini New York, Marekani.
Akiwasilisha hotuba yake, Dkt. Tulia alieleza kuwa kwa zaidi ya robo karne tangu kuanzishwa kwa Azimio la Milenia, ushirikiano kati ya IPU na UN umeonesha mafanikio makubwa, ambapo kwa kila mwaka wameweza kufikia malengo ya kuiwezesha UN kuwa Taasisi inayowajibika, yenye uwazi na inayotekeleza maazimio yake ipasavyo.
Aidha, alibainisha kuwa nafasi ya Mabunge imeainishwa wazi katika lengo namba 55 la Azimio la Pact of the Future, ambalo linaelekeza kuimarisha ushirikiano kati ya Mabunge na Umoja wa Mataifa.
Akisisitiza umuhimu wa wajibu wa Mabunge, Dkt. Tulia alinukuu maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, aliyesema “Inawezekana, tekeleza wajibu wako” akiongeza kuwa Umoja wa Mabunge Duniani unatimiza wajibu wake kuhakikisha kuwa Umoja wa Mataifa unaendelea kuwa imara kwa kupitia Mabunge.
“Dunia inahitaji mabadiliko na sehemu pekee ya kufanya mabadiliko hayo ni ndani ya Umoja wa Mataifa, na wakati wa kufanya hivyo ni sasa,” alisisitiza Dkt. Tulia.
MHE. MAHUNDI AFUNGUA MKUTANO MKUU WATATU WA UMOJA WA MAAFISA UHUSIANO KATIKA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI JIJINI ARUSHA
Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar leo ametembelea mafunzo ya Waandishi Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Halmashauri ya Singida Vijijini mkoani Singida na kuzungumza nao wakati wa mafunzo yao ya siku mbili yaliyoanza leo Septemba 22 na kumalizika kesho Septemba 23, 2022. Akizungumza na Waandishi hao Wasaidizi na Waendesha Vifaa vya Bayometriki Dkt Zakia aliwataka kuzingatia mafunzo wanayopewa, dhamana waliyopewa ya kuendesha zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa weledi. Mafunzo hayo ni…