Author: Mbeya Yetu

Taasisi ya Tulia Trust chini ya Mkurugenzi Wake ambaye ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani(IPU), Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Mbeya Mjini Mhe. Dkt. Tulia Ackson imefanya Ufunguzi wa Mashindano ya Mapishi kwa Mama na Baba Lishe Mbeya Mjini. Mashindano hayo ya Mapishi yanajulikana kwa Jina la Tulia Cooking Festival yanatarajiwa Kufanyika kwa Muda wa Siku Tano (5) hadi siku ya Jumamosi Agosti 31, 2024 katika Viwanja vya Ruanda Nzovwe Mbeya mjini yakishirikisha Washiriki Elfu Moja (1,000) yakiwa na kauli mbiu isemayo *Tumia Nishati Mbadala Kuondoa Uchafuzi wa Mazingira.* Tulia Trust imekuwa…

Read More

Mkuu wa Wilaya ya Songwe amefanya kikao na uongozi wa Kampuni ya Mamba Minerals inayowekeza katika uchimbaji wa madini adimu duniani ya Rare Earth Metals kijiji cha Ngwala Wilayani Songwe.Kikao hicho ambacho pia kimehudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe, ndugu Godfrey Kawacha kimefanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya zilizopo Mkwajuni.Akizungumza baada ya Kikao hicho, Mhe. Itunda amesema kuwa uongozi huo umemweleza maendeleo ya mchakato wa tathmini na mipango ya kuanza kulipa fidia kwa wananchi.Mkuu huyo wa Wilaya ameusisitiza uongozi huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa kila hatua wanayofikia ili wananchi wajue kinachoendelea katika eneo hilo.Pia, DC…

Read More

Shule ya awali na msingi Holy Land ya Makongolosi Chunya Mkoani Mbeya inayonilikiwa na Lawena Nsonda(Baba Mzazi)imefanya mahafali ya kwanza ya darasa la Saba tangu kuanzishwa kwake miaka saba iliyopita mgeni rasmi akiwa ni Titho Tweve. Katika hotuba yake Titho Tweve amewataka wazazi kuwekeza kwenye elimu ili watoto wawe na maisha bora.Aidha Tweve amechangia tani tano za saruji zenye thamani ya shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa uzio kuimarisha usalama wa watoto. Tweve ameupongeza uongozi wa shule ya Holly Land Pre and Primary School kwa namna ilivyojikita kutoa elimu bora hali iliyowafanya wazazi kutoka maeneo mbalimbali nchini kuwaleta…

Read More