Author: Mbeya Yetu

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo Septemba 19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida. Mkoa wa Singida na Dodoma wanataraji kuanza uboreshaji septemba 25 hadi Oktoba mosi mwaka huu.  Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt Zakia Mohamed Abubakar akizungumza wakati alipotembelea mafunzo ya Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida leo Septemba 19, 2024 katika Shule ya Sekondari Mwenge Mkoani Singida.…

Read More

Sharif Abdul Afisa Mwandamizi kitengo cha mahusiano Jamii na ujirani mwema hifadhi ya Taifa Ruaha amesema kupitia mradi wa REGROW wameandaa Muongozo rafiki wa kupokea na kushughulikia malalamiko kutoka kwa wananchi wanaozunguka hifadhi.
Amesema kupitia mradi wa REGROW viongozi na kamati za kushughulikia malalamiko kuanzia ngazi ya Kijiji mpaka mkoa wamejengewa uwezo kwa kupewa elimu namna ya kutumia muongozo huo ili kupokea na kushughulikia malalamiko ya wananchi. Lengo nikuhakikisha wananchi wanaoathirika na shughuli za hifadhi au Mradi wa REGROW wanawasilisha malalamiko yao na yanashughulikiwa kwa utaratibu unaofahamika.
Aidha Abdul amewasihi wananchi wenye malalamiko wafike ofisi za Serikali ya Kijiji nakuwasilisha malalamiko yao au wapige simu ya bure moja kwa moja kwa Hifadhi ya Taifa Ruaha namba 0800110801 na Wizara ya Maliasili na Utalii namba 0800110804 endapo lalamiko linahusu Hifadhi au Mradi wa REGROW. Malalamiko yote yatashughulikiwa kwa usiri na mlalamikaji atalindwa na sheria na tararibu za nchi.

Read More

REGROW ni Mradi wa Serikali unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa Lengo la kuboresha usimamizi wa maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na hifadhi ya Mikumi, Udzungwa na Nyerere wanatekeleza mradi huu. Kutokana na utekelezaji wa mradi wa REGROW au shughuli za Hifadhi ya Taifa Ruaha, unaweza kuwa na maoni au malalamiko yanayotokana na shughuli hizo. Kila mtu ana nafasi ya kutoa malalamiko yake kuhusu changamoto zinazotokana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na shughuli za Mradi wa REGROW. Iwe malalamiko ya athari zinazotokana na usimamizi wa hifadhi, kero za ardhi, unyanyasaji na…

Read More

Naibu Waziri wa Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amehitimisha ziara yake ya siku tatu kutembelea watoa huduma za mawasiliano zilizopo Mkoa wa Dar es Salaam.

Amehitimisha ziara yake kwa kutembelea Kampuni ya TIGO ambapo amefurahishwa na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Kampuni hiyo sanjari na kutoa ajira kwa zaidi ya vijana mia tano.

Amesema uwekezaji uliofanywa unaendana na kasi ya dunia zaidi wakiungana na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha huduma za mawasilano zinatolewa kwa ufanisi mkubwa.

Ziara yake Jijini Dar es Salaam imehusisha Kampuni ya Airtel, Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na kuhitimisha Kampuni ya TIGO

Read More