Author: Mbeya Yetu

REGROW ni Mradi wa Serikali unaofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa Lengo la kuboresha usimamizi wa maliasili na kukuza utalii kusini mwa Tanzania. Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na hifadhi ya Mikumi, Udzungwa na Nyerere wanatekeleza mradi huu. Kutokana na utekelezaji wa mradi wa REGROW au shughuli za Hifadhi ya Taifa Ruaha, unaweza kuwa na maoni au malalamiko yanayotokana na shughuli hizo. Kila mtu ana nafasi ya kutoa malalamiko yake kuhusu changamoto zinazotokana na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na shughuli za Mradi wa REGROW. Iwe malalamiko ya athari zinazotokana na usimamizi wa hifadhi, kero za ardhi, unyanyasaji na…

Read More

Wakazi wa mtaa wa Gombe kusini kata ya Itezi Uyole jijini Mbeya, wanakabiliwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa zaidi ya miaka minne sasa hivyo kuitaka Serikali kutupia jicho kadhia hiyo. Wananchi wa mtaa huo wamesema hayo kwenye ziara ya wataalam wa mamlaka ya maji na usafi wa mazingira Mbeya ambao wamelazimika kutoka ofisini kwenda mtaani kujionea hali halisi ya upatikanaji huduma ya maji na hatua zinazochukuliwa. Wakizungumza mbele ya wataalam hao kwa nyakati tofauti, wananchi hao akiwemo Tuswege Ngondo na Elly Mwampamba, wanasema huduma ya maji wameikosa kwa muda mrefu wengine kwa mwaka mmoja lakini wengine ni zaidi…

Read More

Utalii wa kiutamaduni katika kikundi cha Maasai Boma katika kijiji cha Mikumi Wananchi wa vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Ruaha, Mikumi, Udzungwa  na Nyererevinanufaika na Mradi wa REGROW unaotekelezwa nchinikupitia mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia. Hayo yamesemwa Jijini Mbeya na Bi. Blanka Aquilinus Tengia Naibu Msimamizi wa Mradi wa REGROW unaofadhiliwa na Benki ya Dunia na kutekelezwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na TANAPA, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI), Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Tume ya Taifa ya Umwagiliaji (NIRC) na Bodi ya Bonge la Maji Rufiji (RBWB).Lengo…

Read More

Bi. Betty(Rehema) Fwelefwele Kalala wa Musoma vijijini mkoa wa Mara anamtafuta baba yake mzazi aitwae METHOD KAPINGA kabila Mnyakyusa dini Muislamu anatokea mkoa wa Mbeya. Pia hata familia ya mzee huyo kama atakuwa amefariki. Mzee method kwa sasa umri wake utakuwa kuzidi miaka 75 kama atakuwa bado yupo hai. Mzee Method alimwacha mtoto wake toka akiwa na miezi 3 kuzaliwa. Wajihi wake. Alikuwa na chongo jicho moja na alikuwa anavaa miwani Historia kwa ufupi.Mama wa betty Mama wa Betty anaitwa SARA FWELEFWELE KALALA (yupo hai) alikutana na Method kijijini Butiama mkoa wa Mara mwaka 1976. Bi Sara alikuwa anafanya kazi…

Read More

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson amesema kuwa upo umuhimu mkubwa wa nchi mbalimbali hususani zile zinazounda Umoja wa G7 kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kutafuta usalama duniani na maendeleo ya pamoja na kwamba wakati umefika sasa kwa nchi hizo kushirikiana na nchi za Afrika kama washirika walio sawa. Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 6 Septemba, 2024 wakati akishiriki Mkutano wa 22 wa Maspika wa Mabunge ya nchi za G7 unaofanyika Jijini Verona, nchini Italia ambapo alipata nafasi ya kutoa mitazamo ya IPU…

Read More