Author: Mbeya Yetu

Mkuu wa Wilaya ya Songwe amefanya kikao na uongozi wa Kampuni ya Mamba Minerals inayowekeza katika uchimbaji wa madini adimu duniani ya Rare Earth Metals kijiji cha Ngwala Wilayani Songwe.Kikao hicho ambacho pia kimehudhuriwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Songwe, ndugu Godfrey Kawacha kimefanyika katika ofisi za Mkuu wa Wilaya zilizopo Mkwajuni.Akizungumza baada ya Kikao hicho, Mhe. Itunda amesema kuwa uongozi huo umemweleza maendeleo ya mchakato wa tathmini na mipango ya kuanza kulipa fidia kwa wananchi.Mkuu huyo wa Wilaya ameusisitiza uongozi huo kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kwa kila hatua wanayofikia ili wananchi wajue kinachoendelea katika eneo hilo.Pia, DC…

Read More

Shule ya awali na msingi Holy Land ya Makongolosi Chunya Mkoani Mbeya inayonilikiwa na Lawena Nsonda(Baba Mzazi)imefanya mahafali ya kwanza ya darasa la Saba tangu kuanzishwa kwake miaka saba iliyopita mgeni rasmi akiwa ni Titho Tweve. Katika hotuba yake Titho Tweve amewataka wazazi kuwekeza kwenye elimu ili watoto wawe na maisha bora.Aidha Tweve amechangia tani tano za saruji zenye thamani ya shilingi milioni tano kwa ajili ya ujenzi wa uzio kuimarisha usalama wa watoto. Tweve ameupongeza uongozi wa shule ya Holly Land Pre and Primary School kwa namna ilivyojikita kutoa elimu bora hali iliyowafanya wazazi kutoka maeneo mbalimbali nchini kuwaleta…

Read More

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro akizungumza na Wajumbe kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti matumizi ya ya dawa za kuongeza mbinu haramu michezoni. Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Profesa Hamis Malebo akiwa katika kikao cha Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt Damas Ndumbaro cha kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti matumizi ya dawa za kuongeza mbinu haramu michezoni. *Ni Utekelezaji wa mkataba wa UNESCO Na Mwandishi Wetu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb) ameekutana na wajumbe katika kikao cha kujadili utekelezaji wa Mkataba…

Read More